Chai FM

Maji chanzo zahanati ya Ngeleka kutofunguliwa

10 July 2024, 12:45 pm

Mbunge wa jimbo la Busokelo Mh. Fred Atupele Mwakibete akizungumza na wananchi wa kata ya Kisegese( picha na Lennox Mwamakula)

Na Lennox Mwamakula

Kutokana na kukosekana kwa huduma ya maji katika zahanati ya Ngeleka katika kata ya Kisegese imesababisha zahanati hiyo kutoanza kufanya kazi kwa wakati ambapo mbunge wa jimbo la Busokelo Mh. Fredy Atupele Mwakibete amewaagiza RUWASA kushughulikia suala hilo kwa dharura.

 Akiwa katika ziara ya kata kwa kata kusikiliza changamoto za wananchi katika jimbo la Busokelo Mh. Mwakibete ametoa rai kwa vijana wa kata ya kisegese kujitolea nguvu kazi ili kukamilisha zoezi la upatikanaji wa maji katika zahanati hiyo.

Sauti ya Mbunge Mwakibete kuhusu upatikanaji wa maji Ngeleka
Baadhi ya wananchi wa Kisegese wakifatilia kwa makini mkutano wa Mbunge wa Busokelo (picha na Lennox Mwamakula)

Awali akizungumza katika mkutano huo Fundi wa mradi ameahidi kushughulikia changamoto hiyo kwa wakati ili huduma ya maji ifike katika Zahanati ya Ngeleka.

Sauti ya fundi mkuu wa mradi wa maji Ngeleka

Kwa upande wake mkurugenzi mtendji wa halmashauri ya wilaya ya Busokelo Bi. Loema Pitter ameeleza kwamba ujenzi wa zahanati umekamilika hivyo changamoto ya maji na umeme inafanyiwa kazi ndani ya wiki mkbili kuanzia sasa na kuongeza kwamba kufikia tarehe 20. Julai 2024 huduma za afya zitaanza kutolewa katika zahanati hiyo.

Sauti ya DED Busokelo Bi. Loema pitter

Kwa niaba ya wananchi wa Kisegee diwani wa kata hiyo Bw Lusajo Kala Ameishukuru serikali kwa ujenzi wa zahanati hiyo huku akibainisha baadhi ya changamoto zinazowakabili wananchi hao kuwa ni pamoja na Maji, barabara pamoja na umeme.

Sauti ya Lusajo Kala diwani kata ya Kisegese

Mbunge wa jimbo la Busokelo anaendelea na ziara za kutembelea kata kwa kata kusikiliza na kuzitafutia ufumbuzi changamoto wanazo kabiliana nazo wananchi wa jimbo hilo huku akiwasisitiza wananchi kujitokeza kujiandikisha na kuboresha taarifa zao katika daftari la kudumu la wapiga kura muda utakapo wadia.

Baadhi ya wananchi wa Kisegese wakifuatilia kwa makini mkutano wa Mbunge wa Busokelo Mh. Fredy Atupele Mwakibete (Picha na Lennox Mwamakula)