Madaraka Nyerere: Baba alikuwa hivi.
15 September 2021, 4:12 pm
October 14 mwaka 2020 ilikuwa Kumbukizi ya Kitaifa ya miaka 21 ya kifo cha Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kilichotokea Oktoba 14, 1999 nchini Uingereza alipokuwa anapatiwa matibabu
Mwalimu Nyerere ni mmoja kati ya waasisi wa Taifa la Tanzania, ambaye alishiriki kikamilifu katika harakati za kulikomboa Taifa kutoka kwa ukoloni wa Waingereza
Alikuwa Rais wa kwanza wa Tanganyika na aliongoza tangu Taifa lilipopata Uhuru, Desemba 9, 1961 hadi mwaka 1985
Alikuwa na Falsafa ya Ujamaa na kujitegemea ambapo aliamini ili Taifa liendelee kunahitajika watu, ardhi, Siasa safi na Uongozi bora.
Katika kuadhimisha siku hii kwa kina mwandishi wetu Erick Mallya amefanya mahojiano na Madaraka Nyerere ambaye ni mtoto wa Hayati Mwalimu julius kambarage Nyerere..
Sikiliza hapa sehemu ya Mahojiano kati ya mwandishi wetu Erick Mallya na Mtoto wa hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.