Wadau wa shirika la UZIKWASA wajivunia kubadilishana uzoefu
16 December 2023, 1:58 pm
kukaa kwa pamoja imekuwa ni fursa ya kujifunza kutoka kwa wengine namna ambavyo waliweza kukabiliana na changamoto mbali mbali hali inayowezesha wengine kujifunza jinsi wenzao walivyofanikiwa.
Na Catherine Sekibaha.
Wadau wa washirika la UZIKWASA wamejivunia kubadilishana uzoefu kupitia mbinu wezeshi ambazo zitaimarisha utendaji kazi wao ili kuleta maendeleo kwa jamii.
Bi Consalva Mguluka mdau kutoka shirika la Shalom ambaye ni Afisa Mipango wa shirika hilo amesema kupitia mafunzo ya kubadilishana uzoefu amesema amejifunza mambo mengi yatakayoleta uendelevu wa mbinu wezeshi wanazozitumia ili kuona matunda kwa jamii wanayoihudumia.
Akizungumza kwa niaba ya wadau wengine Ndugu John Masawe kutoka shirika la (HIMD) lililopo Arusha amesema mafunzo hayo yamewawezesha kufanya tathmini ya mwaka mzima ambapo pia ameangalia namna mifumo mbali mbali iliyopo kwenye mashirika yao inavyofanya kazi.
Kwa upande wa Muwezeshaji kutoka shirika la UZIKWASA Ndugu Joseph Peniel amesema kukaa kwa pamoja imekuwa ni fursa ya kujifunza kutoka kwa wengine namna ambavyo waliweza kukabiliana na changamoto mbali mbali na kuwezesha wengine kujifunza jinsi wenzao walivyofanikiwa.
Hayo yamejiri katika Mafunzo ya kubadilishana uzoefu kwa Wadau washirika wa UZIKWASA yaliyofanyika katika kijiji cha Boza kilichopo wilaya ya Pangani Mkoani Tanga.