UZIKWASA yawakutanisha viongozi wa vyombo vya Habari Tanzania
13 March 2023, 2:18 pm
Kwa miaka mingi Shirika la UZIKWASA limekuwa likitoa mafunzo ya ‘mguso’ ambayo yamekuwa yakiwawezesha watu binafsi kutafakari nafasi zao katika kuchochea mabadiliko chanya pamoja na mabadiliko ya kitaasisi na Jamii kwa ujumla.
Na Erick Mallya
Shirika la UZIKWASA lililopo wilayani Pangani Mkoani Tanga kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi na Utamaduni (UNESCO) limeanza rasmi mafunzo maalumu ya siku 4 yanayowakutanisha viongozi waandamizi wa vyombo vya Habari vya Tanzania bara na visiwani yenye lengo la ‘kuwezeshana kwa pamoja kama viongozi wa vyombo vya Habari juu ya kutafakari na kuzingatia masuala ya jinsia kwa kutumia mbinu wezeshi (Mguso)‘
Mafunzo hayo yanaendelea katika moja ya kumbi za Royal Village zilizopo jijini Dodoma kuanzia Machi 13-16, 2023.
Kwa miaka mingi shirika la UZIKWASA limekuwa likitoa mafunzo ya mguso ambayo yamekuwa yakiwawezesha watu binafsi kutakari nafasi zao katika kuchochea mabadiliko chanya pamoja na mabadiliko ya kitaasisi.
Wanufaika wa mafunzo hayo wamekuwa vongozi wa dini, viongozi wa taasisi, waandishi wa habari, vongozi wa kisiasa na wale wanaosimamia masuala ya Jinsia na Mazingira.
Faida za mafunzo hayo zimetambulika katika ngazi ya Kitaifa na Kimataifa.
Mafunzo hayo yanatarajiwa pia kuwajengea viongozi hao uwezo wa kujtathmini, kusikiliza,kuwajibika,kuwawezesha wengine kuwa kufikia uwezo wao na kufanya kazi katika mazingira ya timu, kuboresha mahusiano na mawasiliano na kutengeneza maswali ya kimkakati ili kuhakikisha masuala ya Jinsia yanazinagtiwa ndani na nje ya vyombo vya Habari.
Vongozi hawa wa vyombo vya Habari wanatarajiwa kuwa sehemu ya uwezeshaji wa waandishi wa habari katika umahiri wa kufanya kazi zao kwa kuzingatia masuala ya jinsia ndani nan je ya vyombo vya Habari.
Mafunzo hayo yatafuatiwa na mafunzo kwa waandishi wa Habari wa vituo 15 vya Tanzania bara na visiwani baadae juma hili.