Pangani FM

Aweso aungana na waumini wa dini ya kiislamu Pangani kwenye maulid

15 February 2025, 9:58 pm

Pichani mbunge wa Jimbo la Pangani na waziri wa maji Mhe. Juma Hamidu Aweso akiwa katikati ya waumini wa kiislamu katika maulid ya mazazi ya Mtume Mohammad S.A.W iliyofanyika katika madrasa tul jumuiya BAKWATA mjini Pangani viongozi wa kiserikali, dini na watu mashuhuri walihudhuria.

Maulid hiyo imefanyika tarehe 14 february 2025 sawa na mwezi kumi na tano shaban kwa mwaka wa kiislamu ikienda sambamba na kufunga masomo.

Na Hamisi Makungu

Waumini wa Dini ya Kiislamu na watanzania wote wamehimizwa kujifunza na kuziishi tabia njema ikiwemo kuwa na subra, upole, huruma na uadilifu kutoka kwa kiongozi wa umma huu Mtume Muhammad S.A.W.

Hayo yamejiri katika sherehe za maulidi ya kuadhimisha mazazi ya Mtume Muhammad S.A.W katika Madrasatul Jumuiyatul Islamiyya BAKWATA Mjini Pangani, sherehe ambazo zimehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa dini kutoka ndani na nje ya Tanzania, viongozi wa Serikali na kisiasa.

Mwandishi wetu KHAMISI MAKUNGU ametuandalia taarifa ifuatayo.

Sikiliza hapa