Wazazi shirikianeni katika malezi ya watoto wenu wapate elimu bora
25 October 2023, 12:18 pm
Kila mmoja akisimama katika nafasi yake itapunguza wanafunzi kuzurura mitaani na kuacha utoro.
Na Saa Zumo.
Wazazi na walezi wameshauriwa kuwa na ushirikiano katika malezi na makuzi ya watoto ili kuwawezesha kusoma kwa bidii na kufikia malengo yao.
Hayo yamejiri katika kipindi cha Kumbe na Mimi kinachorushwa na kituo hiki ikiwa ni mjadala juu ya jitihada za wazazi na viongozi kutokomeza utoro kwa wanafunzi mashuleni.
Akizungumza kwenye mjadala huo Diwani kata ya Kimang’a Mh. Salimu Mwandaro amesema kila mmoja akisimama katika nafasi yake itapunguza wanafunzi kuzurura mitaani na kuacha utoro.
Pili Yusuph mmoja ya wazazi akizungumza katika Mjadala huo amesema wazazi na walezi wana jukumu la kuhakikisha wana wanunulia watoto wao mahitaji muhimu.
Hata hivyo Muheshimiwa Mwandaro Diwani wa Kata ya Kimang’a amesema kuwa nguvu zilizowekezwa na Serikali katika ujenzi wa Miundombinu ya elimu ni kubwa hivyo wazazi wana wajibu wa kuhakikisha Watoto wao wanasoma.