BOOST, EP4R na TEA zaing’arisha shule ya msingi Pangani
25 October 2023, 11:39 am
Serikali kupitia viongozi wetu wametuheshimisha, madarasa yaliyojengwa yatakuwa msaada mkubwa kwa wanafunzi.
Na Cosmas Clement.
Serikali imefanikiwa kutumia zaidi ya shilingi milioni 100 kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2020/21 hadi 2022/23 kwa ajili kutekeleza ujenzi wa miundombinu ya madarasa na matundu ya vyoo katika shule ya msingi Pangani iliyopo mkoani Tanga.
Hayo yamezungumzwa na Mwalimu Mkuu shule hiyo Hamis Nuru amnaye amesema pesa hizo zimetoka katika miradi ya Boost, EP4R, pamoja na taasisi ya elimu Tanzania na kutekelezwa katika awamu tatu.
Mwalimu Hamisi amesema kuwa ujenzi wa madarasa hayo utasaidia kupunguza mrundikano wa wanafunzi pindi idadi ya walimu itakapoongezwa shuleni hapo.
Baadhi ya walimu shuleni hapo wameishukuru serikali kwa kutekeleza mradi wa choo cha walimu hao kwani hapo awali walikuwa wakipata adha ya huduma hiyo.
Serikali imekuwa ikitekeleza ujenzi wa miundombinu mashuleni hali inayotarajiwa kupunguza changamoto hususani kwa shule zilizokuwa na changamoto ya uhaba madarasa au uchakavu wa majengo.