Wanafunzi tisa wakumbwa na kamata kamata utoro sugu katika kijiji cha Kimang’a
13 October 2023, 5:17 pm
“Tumeanza na Wanafunzi wa Shule za Msingi kwasasa tatizo hilo limepungutunajipanga kukabiliana na tatizo la utoro kwa wanafunzi wa sekondari” Diwani kata ya Kimang’a Mheshimiwa SALIMU MWANDARO
Na Saa Zumo
Wanafunzi tisa wanaosoma elimu ya Sekondari katika Kijiji cha Kimang’a wamekumbwa na kamata kamata ya utoro sugu mashuleni.
Wengi wa wanafunzi hao ni wa kidato cha kwanza katika Shule ya Sekondari Pangani Halisi ambapo msako wa nyumba kwa nyumba umefanywa na Polisi jamii kwa lengo la kuwabaini wanafunzi hao na kuwataka kutoa maelezo ya kwanini hawaudhurii masomo.
Akizungumza na Pangani Fm Diwani kata ya Kimang’a Mheshimiwa SALIMU MWANDARO amesema lengo la zoezi hilo ni kupunguza utoro mashuleni huku akisema sababu za kutokuhudhuria shuleni wanazozitaja wanafunzi hao hazina tija.
Baadhi ya wazazi ambao watoto wao wamekumbwa na msako huo wameahidi kutoa ushirikiano ili watoto wao waweze kurejea shuleni huku wakitoa shukurani kwa viongozi kwa hatua waliochukua dhidi ya watoto wao.
Ili kufanikisha zoezi la wanafunzi hao kuudhuria masomo bila kukosa Mheshimiwa MWANDARO amesema kutakuwa na uangalizi maalumu kwa ushirikiano kati ya viongozi na wazazi wa kata hiyo.