Wadau wa sekta ya uvuvi Pangani watakiwa kushirikiana kulinda rasilimali za bahari
9 October 2023, 2:36 pm
“Tungekuwa tumepata elimu mapema, tungejua wa kulia nae”
Na Abdilhalim Shukran
Wataalamu wa sekta ya Uvivi wilayani Pangani wametakiwa kushirikiana na wavuvi kuimarisha jitihada za kulinda rasilimali za bahari.
Ushauri huo umetolewa na wadau wa sekta ya uvuvi katika wilaya ya Pangani wakati wakichangia mada kupitia kipindi cha “Nitunze Nikutunze” kinachorushwa na kituo cha redio cha Pangani Fm.
Katika hatua nyingine wadau hao wamesema suala la kulinda na Uvuvi haramu unavyofanywa na baadhi ya wavuvi unachangiwa na kukosekana kwa ushirikiano kati ya wavuvi na wataalamu wa sekta hiyo
Kwa upande wake Afisa Uvuvi Wilaya Pangani JOEL MABAGALA amehidi kuzifanyia kazi changamoto zilizotolewa na wavuvi hao huku akiwasihi kufata sheria na taratibu za uvuvi kama zilivyo Pangwa.
Pamoja na kuhidi kuyafanyia kazi mapendeko ya wavuvi Bwana JOEL amewataka wavuvi kujiunga katika vyama vya uvuvi na ushirika ili waweze kupata fursa zinazotolewa na serikali na wadau wengine wa sekta ya hiyo.