Pangani FM
Pangani watakiwa kutibu maji ya mvua kabla ya kuyatumia
6 October 2023, 2:25 pm
Maji ya mvua yanakuwa salama iwapo tu yatakingwa moja kwa moja wakati wa mvua.
Na Mariam Ally
Wananchi wilayani Pangani Mkoani Tanga wametakiwa kuyatibu maji ya mnvua kabla ya kutumia na kuepukana na dhana kuwa maji hayo ni salama wakati wote.
Hayo yameelezwa na afisa afya wilaya ya Pangani Bi Mwanahamisi Ramadhani ambapo amesema maji yamvua yanakuwa salama iwapo tu yatakingwa moja kwa moja wakati wa mvua.
Bi mwanahamisi ameeleza njia ambazo mwananchi anaweza kuzitumia kutibu maji ya mvua ili yaweze kuwa salama kwa mnywaji.
Kumekuwa na kawaida ya jamii kuamini kwamba maji ya mvua ni salama na wengi kuyatumia kwa ajili ya kunywa.