Tree of Hope wabaini haya Pangani
27 March 2023, 12:23 pm
Shirika lisilo la Kiserikali TREE OF HOPE lenye makao yake makuu
jijini Tanga limekutana na wadau wa elimu katika vijiji vya Ubangaa,
Stahabu, Kipumbwi na Mkalamo katika mdahalo uliolenga kujadili
changamoto za elimu wilayani Pangani.
Akizungumza na Pangani FM baada ya mdahalo huo Afisa Programu kutoka shirika hilo Bw. GoodluckMalilo amesema katika siku hizo mbili
ya midahalo wamefanikiwa kubaini mafanikio ya kuandikishwa shule
kwa Watoto wenye ulemavu, pamoja na wazazi kuchangia walimu wa
kujitolea.
Bwana Malilo amesema kuwa kutokana na mdahalo huo wamebaini kuna
changamoto ya kutokuwa na walimu mahsusi wa watoto wenye mahitaji
maalumu katika shule zilizopo katika vijiji hivyo.
Awali wakizungumza wakati wa mawasilisho washiriki katika mdahalo
huo, wa vijiji vilivyotembelewa wameeleze jinsi mradi wa uwajibikaji,
na elimu jumuishi umewawezesha wao kujitambua na kuona wanao
wajibu wa kushughulikia changamoto za elimu zilizopo vijijini kwao .
Shirika la Tree of Hope inaendesha mradi unaolenga uwajibikaji,
uboreshaji wa elimu na elimu jumuishi kwa vijiji vinne, huku katika
Mdahalo huo wa siku mbili Jumatano na Alhamisi ukiwashirikisha
wadau mbalimbali ikiwemo viongozi wa vijiji, walimu, waratibu elimu
kata, maafisa maendeleo kata, viongozi wa dini na wananchi.