Wakufunzi 10 kubadili vyombo vya habari kijinsia
17 March 2023, 3:08 pm
Na Erick Mallya
Shirika la UZIKWASA lililopo wilayani Pangani Mkoani Tanga kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi na Utamaduni (UNESCO) limehitimisha mafunzo maalumu ya siku 4 yaliyowakutanisha viongozi waandamizi wa vyombo vya Habari vya Tanzania bara na visiwani.
Viongozi hao ambao idadi yao ni 10 wamepatiwa mafunzo ya wakufunzi (ToTs) ili kuwapa mbinu mbalimbali za kuwawezesha wengine kwenye vituo vyao katika Kuimarisha utangazaji wa jinsia ndani na kupitia vyombo vya Habari.
Mafunzo hayo yamefanyika katika moja ya Kumbi za mikutano za Royal Village zilizopo jijini Dodoma kuanzia Jumatatu Machi 13 hadi 16, 2023.
Wakizungumza mara baada ya kukamilika kwa mafunzo hayo washiriki hao wametoa shukrani zao kwenda kwa Shirika la UZIKWASA kutokana na mbnu za Kiuongozi walizozipata.
Nawashukuru sana kwa mafunzo haya ambayo yana mbinu wezeshi zilizonisaidia kujiona na kujitafakari, wakati nafikiria safari yangu ya uongozi nimegundua kuwa nimesababsisha maumivu
Zania Kweka wa Dodoma FM
Kwa miaka mingi Shirika la UZIKWASA limekuwa likitoa mafunzo ya ‘mguso’ ambayo yamekuwa yakiwawezesha watu binafsi kutafakari nafasi zao katika kuchochea mabadiliko chanya pamoja na mabadiliko ya kitaasisi na Jamii kwa ujumla.
Wanufaika wa mafunzo hayo wamekuwa vongozi wa dini, viongozi wa taasisi, waandishi wa habari, vongozi wa kisiasa na wale wanaosimamia masuala ya Jinsia na Mazingira.
Faida za mafunzo hayo zimetambulika katika ngazi ya Kitaifa na Kimataifa.