Barabara ya Lami Tanga-Pangani hii hapa.
1 March 2023, 1:53 pm
Barabara ya Tanga-Pangani KM 50, ni sehemu ya barabara ya Tanga- Pangani- Saadani -Bagamoyo yenye urefu wa KM 256 ambayo ni sehemu ya barabara kuu ya Horohoro-Tanga- Pangani- Saadani – Bagamoyo hadi Dar es Salaam kwa upande wa Tanzania na Malindi-Mombasa hadi Lungalunga nchini Kenya ambayo ina lengo la kurahisisha usafirishaji wa mizigo, biashara za mipakani na kukuza utalii itakapokamilika.
Na Erick Mallya
Ujenzi wa barabara ya Tanga-Pangani Saadan-Bagamoyo kwa kiwango cha lami unatarajiwa kukamilika mwezi Machi mwaka 2025.
Mkuu wa wilaya ya Pangani Bi. Zainab Abdallah ameyasema hayo katika majojiano maalumu aliyofanya na Pangani FM jana katika Studo za kituo hicho.
Mungu akijalia mwaka huu kipande cha Kilomita 50 utakamilika mwaka huu Tanga-Pangani Kilomita 50 inaenda kuwa na kiwango cha Lami.
Amesema Bi Zainab Abdallah
Bi Zainab Abdallah amesema ujenzi wa awamu ya kwanza ni ujenzi wa kipande cha Kilometa 50 kutoka Pangani-Tanga ambao unatarajiwa kukamlika mwaka huu.