Polisi Muheza waingilia kati utoro unaosababishwa na Machungwa
25 February 2023, 4:50 pm
Na Saa Zumo
Baadhi ya vijana wilayani Muheza Mkoani Tanga wamekumbwa na tabia ya kutotilia mkazo suala la Elimu na kukimbilia katika biashara ya uuzaji wa machungwa.
Kutokana na wilaya hiyo kuzalisha kwa wingi machugwa zao hilo ni rahisi kupatikana hata kwa vijana wasio na mashamba.
Vijana wengi wa muheza wameona utajiri ni machungwa, ukimuuliza unataka nini anakuambia anataka kulima.
Hali hiyo imepelekea kuongezeka kwa vitendo vya utoro mashuleni na kutokaa na vijana hao kutokuwa wamiliki wa mashamba wamekuwa wakijipatia machungwa kw akuiba mashambani kasha kuyauza maeneo mbalimbali hsusani pembezoni mwa barabara ya kwenda mikoani.
Pangani FM imefika katika kitu cha Polisi cha Muheza na kuzungumza na Mkuu wa kituo hicho Bi Kuluthumu Husein Bambe ambaye amesema kuwa kufuatia hali hiyo jeshi la polisi limekuwa na kampeni ya kuwaelimisha vijana hao ili kuachana na tabia hiyo.
Ukimuhoji mtoto kwa nini hutaki shule anakujibu kuwa nikienda huwa sielewi.
Vijana wengi wa wilaya ya muheza kikubwa ambacho tumebaini mimi kama mkuu wa kituo, ni ukosefu wa elimu, vijana wengi wa muheza wameona utajiri ni machungwa kwa hiyo unakuta mtu anakuambia mimi sitaki shule, ukimuuliza unataka nini anakuambia anataka kulima hapo unajiuliza kwa umri wake mwanafunzi wa kidato cha pili atalima heka ngapi ili aweze kupata kipato, kwa hiyo tunatumia nguvu nyingi kuwalazimisha vijana warudi shule Amesema Kamanda Bambe
BI kuluthumu bambe amesema kuwa hayo yanajiri kutokana na baadhi ya wazazi kushindwa kusimama na kuhamasisha watoto ili kupunguza vitendo vya utoro mashuleni.