Wakulima Pangani kupima hali ya Udongo wa Mashamba yao.
30 June 2022, 11:11 am
Wakulima wilayani Pangani mkoani Tanga wameshauriwa kuwa na utaratibu wa kupima hali ya afya ya udongo katika mashamba yao ili kutambua njia bora ya kusimamia ukuaji wa mazao yao na kuongeza tija katika shughuli zao za kilimo.
Hayo yamezungumza na Dk. Sibaway Mwango ambaye ni mtafiti mkuu kitaifa kutoka kituo cha utafiti wa kilimo TARI kilichopo Mlingano ambapo amesema kuwa upimaji wa udongo unamuwezesha mkulima kufanya maamuzi sahihi zaidi kwenye Shamba lake.
Dk. Mwango amesema kwa mkulima anayehitaji kupima afya ya udongo wa shamba lake anapaswa kuwasiliana na wataalamu wa maabara ya TARI au kuwasiliana na maafisa ugani waliopo katika maeneo yao.
Dk. Mwango amesema kwa mkulima anayehitaji kupima afya ya udongo wa shamba lake anapaswa kuwasiliana na wataalamu wa maabara ya TARI au kuwasiliana na maafisa ugani waliopo katika maeneo yao.
Kufuatia hayo Pangani FM imezungumza na Afisa Kilimo wilaya ya Pangani Bw. Ramadhani Zuberi ambaye amedai kuwa idara yake inatarajia kuanza kupima hali ya afya ya udongo mara baada ya kupokea vifaa vya upimaji kutoka wizara ya kilimo.
Faida za kupima udongo kwa mkulima ni pamoja na kujua ni aina gani ya udongo uliopo katika eneo husika ,ni aina gazi ya zao ambalo linaweza kustawi katika udongo huo ,udongo huo unahitaji mbolea au hauitaji pamoja na kujua aina ya mazao yanayofaa katika shamba la mkulima, kujua virutubishi vilivyopo katika udongo na ni kwa kiasi gani, pamoja na mkulima kununua mbolea kulingana na upungufu wa virutubishi vinavyohitajika kwenye udongo.