Kuelekea ziara ya Makamu wa Rais Tanga,RC Shigela atembelea Mradi ya Maji Korogwe.
10 March 2021, 10:41 am
Mkuu wa Mkoa Tanga Mh.Martine Shigela akiwa na Kamati ya usalama ya Mkoa na wilaya ametembelea na kujionea ukamilifu wa Mradi wa Maji unaounganisha vijiji vya Kwasunga mpirani kata ya Makuyuni na Kwasung_A kilichopo kata ya Magiragereza wilayani Korogwe Mkoani Tanga
Mradi huo una thamani ya Tsh.Mil.290 na matenki mawili ya jumla lita laki moja na elfu hamsini sambamba na vituo 20 vya wanachi kupata maji.
LKatika ziara hiyo Mkuu wa Mkoa amepokelewa na Wanachi ambao wamemshukuru na kutuma Shukrani zao kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.John Pombe Magufuli pamoja na usimamizi na ufuatiliaji mzuri unaofanywa na Waziri wa Maji Mh.Jumaa Aweso (MB PANGANI).
Mradi huu ni sehemu ya miradi itakayozunduliwa na Mh.Makamu wa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anaetarajia kuwa na ziara ya kikazi mkoani Tanga hivi karibuni.