Lumuli kuwamlika watoto yatima Rungwe
15 September 2023, 12:58 pm
Jamii inatakiwa kuwalea na kuwalinda watoto yatima katika maeneo yao ikiwa ni pamoja na kuwalea katika mazingira yenye usalama kwao.
Na Lennox Mwamakula
Ili kukabiliana na wimbi la watoto waishio katika mazingira magumu uongozi wa kijiji na kata ya Ndanto wilayani Rungwe mkoani Mbeya umesema unaendelea kukabiliana nao ili taifa liweze kuwa salama na kuwa na kizazi chenye maadili mema.
Kauli hiyo imetolewa na diwani wa kata ya Ndanto Mh, Samwel Mwinuka kwenye hafla ya uzinduzi wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Lumuli [lumuli orphans] Kilichopo kijiji cha Ntokela wilayani Rungwe ambapo amesema mtoto ni zawadi kutoka kwa Mungu hivyo kila mmoja anao wajibu wa kuwalea katika misingi bora.
Akisoma Risala mbele ya Mgeni rasmi mwenyekiti wa bodi ya kituo hicho ndg. Luka Kyando amezitaja changamoto ambazo kituo kinakabiliwa nazo kuwa ni pamoja na ukosefu wa vifaa vya kuchezea pamoja na vifaa vya ofisini kama vile komputa.
Aidha Kyando ameeleza kuwa kituo hicho kinatarajia kuwa na miradi mbalimbali ili kuwezesha watoto hao kupata chakula cha kutosha pamoja na mahitaji mengine ya msingi ikiwemo elimu.
Akijibu Risala hiyo mgeni Rasmi Mh. Mwinuka ambaye ni diwani wa kata ya Ndanto ameahidi kutoa ushirikiano kwa kituo hicho huku akiahidi kwamba serikali pia itaunga mkono jitihada hizo.
Diwani wa viti maalum tarafa ya Ukukwe Elizabeth Ngaga kuwa mvumilivu na kumuomba Mungu kwani kazi ya kulea watoto yatima inahitaji moyo wa unyenyekevu na huruma.
Akitoa neno la shukurani kwa niaba ya mkurugenzi wa kituo hicho Efeso Joseph Tweve ameiomba jamii ya Rungwe na maeneojirani kutoa ushirikiano zaidi kw kituo hicho kwa maslahi mapana ya watoto hao.