Zaidi ya kiasi cha shilingi Billion 60, 672,404,687.00 kimependekezwa kwa mwaka wa fedha 2024/2025 Rungwe
30 January 2024, 5:51 pm
Halmashauri imejizatiti kukusanya zaidi ya kiasi cha shilingi bilioni 60.672 ili kuendelea kukamilisha miradi yote ya kipaombele na kuwaondolea changamoto wakazi wa Rungwe
Kikao maalumu cha Baraza la Madiwani kimeketi leo tarehe 30.01.2024 lengo kuu likiwa ni kupitia na kupitisha Rasimu ya bajeti kwa mwaka wa fedha 2024/25.
Katika kikao hiki Baraza limepitisha Rasimu ya Shilingi Billion 60, 672,404,687.00 huku vipaumbele kwa mwaka wa fedha 2024/25 vikiwa ni:
Akisoma taarifa mbele ya kikao cha madiwani mwenyekiti wa baraza hilo mpokigwa mwankuga amesema vipaombele hivyo vilivyoaainishwa kwenye rasmu hiyo vitaenda kuondoa kero za wananchi kwa kiasi kikubwa
Sauti ya mwankuga
1.Kuimarisha Mapato ya Ndani kwa kubuni vyanzo vipya
2.Kuimarisha miundombinu ya Biashara na Masoko ili kujenga mazingira mazuri ya biashara na ukusanyaji wa mapato.
3. kuboresha miundombinu ya elimu na afya
4.Kuboresha mazingira ya Uwekezaji kwa kuendekeleza maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya uwekezaji ili kukuza uchumi wa jamii na taifa kwa ujumla.
5.Kuboresha Mazingira ya kufanya kazi kwa watumishi.
6.Ununuzi wa gari jipya la taka na mengine mawili kwa ajili ya shughuli za utawala na usimamizi pamoja na ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo.
Katika mwaka wa fedha uliopita Halmashauri ilipanga kukusanya na kutumia kiasi cha shilingi Billion 59,568,016,000.00
Huku mwaka wa fedha ukiwa haujaisha bajeti imetekelezwa kwa mafanikio makubwa. Baadhi yake ni pamoja na :
1 .Ununuzi wa gari moja (Tipper) tani 10 kwa ajili ya usafirishaji wa taka ngumu.
2.Halmashauri imezalisha miche ya miti 125,200 inayolinda vyanzo vya maji, mbao, vivuli na matunda.
3. Halmashauri imefanikiwa kuchangia kiasi cha shilingi 234,890,000 kutokana na mapato ya ndani kwenye mfuko wa Wanawake, vijana na watu wenye ulemavu. Kiasi cha shilingi million 84,354,400 kimekusanywa kutokana na marejesho ya vikundi.
4.Halmashauri imefanikiwa kuhimilisha jumla ya ng’ombe 4000 kwa ajili kupanua upatikanaji wa Maziwa na mifugo bora.
5.Halmashauri imefanikiwa kujenga stendi mpya ya magari madogo ya abiria kwa kiwango cha Paving blocks katika mji wa Tukuyu.
6.Halmashauri imefanikiwa kujenga vyumba 04 vya madarasa, Ofisi, Vyoo katika shule ya mchepuo wa kiingereza iliyopo Ilenge. Pamoja na ujenzi wa kituo cha afya Kinyala kwa kutumia mapato ya ndani.
7.Halmashauri imefanikiwa kupokea kiasi cha shilingi 2,800,000,0000 kwa ajili ya ukamilishaji jengo la wagonjwa wa nje katika hospitali ya wilaya, pamoja na ujenzi wa vituo vya afya Masoko na Kiwira.
8.Halmashauri imefanikiwa kujenga na kusajili shule mpya ya msingi Kibumbe na Sekondari ya Lupepo.