Sibuka FM
Sibuka FM
25 August 2025, 1:01 pm

“Walezi/Wazazi tunalo jukumu kubwa la kuwalinda watoto wetu wakati wote bila kujali mazingira waliyopo ili kuwakinga na vitu vinyoweza kuzuilika maana watoto ni tunu ya taifa lijalo”.
Na,Anitha Balingilaki
Watoto watatu wa kutoka kwenye familia tatu wawili wakiwa wa kitongoji kimoja wamefariki dunia kwa kukosa hewa baada ya kujifungia kwenye tent ambalo ndani yake waliweka jiko la mkaa na tukio hilo limetokea kata ya Mkula wilayani Busega mkoani Simiyu.
Watoto hao walikuwa kwenye makambi ya waadventista na waliwasha jiko hili kupika uji na badae mvua ilianza kunyesha wakajifungia ndani ya tenti ambalo ndani yake kulikuwa na jiko la mkaa wakiwa na lengo la kuepuka baridi.
Wakizungumza na Sibuka fm, Esta Bugoye bibi wa marehemu Loveness,Yusuph Lameck Mzazi wa marehemu Passion na Veronica Paul bibi yake marehemu Marry wameeleza namna walivyopokea taarifa hizo.
Wakizungumzia tukio hilo Mahangi Luhanya mkazi wa Mkula na Lucas Mashauri wametoa ushauri kwa jamii kwa kila tent liwe na msimamizi ambaye ni mtu mzima wanapokuwa kwenye makambi yoyote ili kuepusha changamoto zinazoweza kuepukika.
Tukio hilo limethibitishwa na mkuu wa mkoa wa Simiyu Annamringi Macha na kuwataja watoto hao kwa majina yao,Loveness Emmanuel Kilonzo alikuwa mwanafunzi wa darasa la tatu (9) Passion Yusuph alikuwa mwanafunzi wa darasa la saba (14) na Mary Jackson (12).