

20 March 2025, 1:23 pm
Baada ya Serikali kujenga Mradi na kuukadhi kwenu, Jukumu la kuulinda na Kuutunza ni lakwenu wananchi wenyewe , hivyo niwaomba wananchi wa Ipililo lindeni miundombinu ya Maji katika Mradi huu, asitokee mwananchi mmoja akaja kukata mabomba halafu nyie mnamuangalia tu. kila mmoja ahusike katika kulinda ” DC Anna Gidarya “
Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Maswa ambaye ni Mkuu wa Wilaya Itilima Mkoani Simiyu Mhe, Anna Gidarya amewataka wanachi wa Kijiji cha Ipililo Kata ya Ipililo kuhakikisha wanatunza Miundombinu ya Maji katika Mradi huo ili uendelee kunufaisha vizazi vijavyo.
Mhe Gidarya amesema hayo wakati wa kuweka Jiwe la Msingi katika Ujenzi wa Mradi wa Maji unaogharimu zaidi ya Bilioni 1. 3 na kusema kuwa suala la kutunza Mradi ni jukumu la wananchi mwenyewe.
Amesema kuwa kwa sasa Mradi upo katika hatua za mwisho za Ukamilishaji , katika kipindi hiki cha matazamio wananchi wataendelea kuchota maji bure huku akiwapongeza Ruwasa wilaya ya Maswa kwa Usimamizi Mzuri wa Mradi huo unaoenda kumtua mama ndoo kichwani.
Akitoa taarifa kwa Mgeni rasmi, kaimu meneja wa wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (ruwasa ) wilayani Maswa Mhandisi Jofrey Kiama amesema kuwa lengo la Mradi ni kutoa huduma ya Maji kwa wananchi wa Ipililo huku akisema ushirikishwaji wa jamii ukiwa umezingatiwa.
Akizungumza kwa niaba ya Mbunge wa Jimbo Maswa Mashariki katibu wa Mbunge huyo Ndugu Marco Bukwimba amesema suala la Maji katika kijiji cha Ipililo lilikuwa linamnyima Usingizi lakini kwa sasa ameutua huo mzigo aliokuwa ameubeba kwa Muda mrefu Mhe Mbunge Stanslaus Nyongo.
Diwani wa Viti maalumu ccm kata ya Ipililo Mhe Modester Mussa Kabeya kwa niaba ya wananchi wa Ipililo amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassani kwa kutoa Fedha ili kujenga Mradi wa Maji katika kijiji hicho kwani wananchi walikuwa wakipata adha kubwa ya kuamka Usiku kwenda kutafuta Maji