Sibuka FM

Pelekeni watoto shule wakasome, DC Simalenga

10 April 2026, 6:59 am

Pichani ni mkuu wa wilaya ya Bariadi, Simon Simalenga akizungumza jambo kwenye mkutano na wananchi, hawapo pichani. Picha kutoka maktaba ya Sibuka fm

Waswahili na wajuzi wa falsafa wanamisemo mizuri kuhusu elimu utasikia elimu ni bahari elimu ni ufunguo wa maisha, elimu haina mwisho, elimu ni dira hiyo yote misemo ni chachu ya kuleta ushindani na hamasa kwa wazazi na walezi kujuwa umuhimu wa elimu kwa dunia hii ambayo imejaa teknolojia”.

Na Daniel Manyanga 

Mkuu wa wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu, Simon Simalenga amewataka wazazi na walezi wilayani humo kuhakikisha watoto wao wenye umri wa kwenda shuleni wanakwenda shuleni kusoma badala ya kwenda kuchunga mifugo, kulima na kufanya kazi za ndani ili waweze kutimiza ndoto zao kielimu.

Simalenga ametoa rai hiyo wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Kilalo katika halmashauri ya wilaya ya Bariadi ambapo amesema kuwa serikali imefanya uwekezaji na maboresho makubwa katika sekta ya elimu hivyo ni muhimu watoto wakapatiwa fursa ya elimu ili kuondokana na ujinga.

Sauti ya mkuu wa wilaya ya Bariadi Simon Simalenga

Akizungumza katika mkutano huo mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Bariadi Mayala Lucas amesema kuwa halmashauri hiyo imeendelea kufanya vuzuri katika sekta ya elimu huku akiwataka wazazi kutowabagua watoto wenye ulemavu na wakike badala yake wawapeleke shuleni wote kupata elimu.

Sauti ya mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Bariadi, Mayala Lucas