Sibuka FM

TANROADS Simiyu waanza ujenzi wa barabara ya heavy weight

18 March 2026, 4:43 pm

Pichani aliyesimama ni mkuu wa mkoa wa Simiyu, Anamringi Macha akizungumza na wajumbe katika kikao Picha kwa hisani ya ofisi ya mkuu wa mkoa wa Simiyu

“Tunahitaji kuwa na miundombinu imara ya barabara ili kulinda usalama wa vyombo vya usafiri pamoja na watumiaji wake maana siku hizi kelele zimekuwa nyingi sana kutoka kwa watumiaji wa barabara juu ya ubovu wake na namna ambavyo unachangia kuhari vyombo vyao vya usafiri”. 

Na,Daniel Manyanga 

Kufuatia malalamiko ya mara kwa mara ya wananchi na watumiaji wa barabara kuu ya mkoa wa Simiyu kutoka Mwigumbi,Maswa ,Bariadi na Busega inayounganisha mikoa ya Mara,Shinyanga na Mwanza kuwa mbovu wakala wa barabra Tanzania (TANROADS) mkoa wa Simiyu wameanza kufanya ukarabati wa barabara hiyo ili kuwaondolea kero mbalimbali zinazowakabili watumiaji wa barabara hiyo.

Akizungumza baada ya kuanza kwa matengenezo hayo mhandisi Boniphace Mkumbo meneja wa wakala wa barabara Tanzania (TANROADS) mkoa wa Simiyu amesema kuwa ukarabati huo unaofanywa kwa sasa tofauti na walivyokuwa wakifanya hapo awali na jinsi utakavyosaidia kuimarisha barabara hiyo ili kuondoa changamoto kwa watumiaji wa miundombinu hiyo.

Sauti ya meneja wa TANROADS mkoa wa Simiyu, Mhandisi Boniphace Mkumbo

Wakizungumza na Sibuka Fm baadhi watumiaji wa barabara hiyo Godfrey Mgosi, Aisha Chamari na Paschal Balina wanaeleza adha watakazoziepuka baada ya ukarabati huo kukamilika.

Sauti ya wananchi na watumiaji wa miundombinu hiyo

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Simiyu, Anamringi Macha akatoa maelekezo ya serikali juu ya ukarabati wa barabara hiyo unaoendelea.

Sauti ya mkuu wa mkoa wa Simiyu Anamringi Macha