Sibuka FM
Sibuka FM
17 March 2026, 6:19 am

“Mkuu wa mkoa wa Simiyu Anamringi Macha ameagiza watu wote wanoharibu miundombinu ya barabara kwa namna mbalimbali ikiwemo kupitisha mifugo kwenye barabara za lami mkoani humo wapatiwe elimu juu ya matumizi ya barabara na baada ya kuelemishwa wale wote watakaoendelea kufanya shughuli zinazoharibu miundombinu hiyo wachukuliwe hatua”.
Na,Daniel Manyanga
Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Anamringi Macha ameziagiza mamlaka za barabara tutoa elimu ya matumizi ya miundombinu hiyo kabla ya kuchukua hatua kali za kisheria kwa watu wanaoharibu barabara kupitia shughuli mbalimbali wanazofanya kama kupitisha Mifugo kwenye lami.
Anamringi Macha ametoa maagizo hayo wakati akizungumza katika kikao cha bodi ya barabara mkoani hapo ambapo amesema kuwa kuna kila haja kwa mamlaka kutoa elimu ya matumizi ya barabara za lami hasa kwa wananchi na kutokana na jamii kubwa mkoani hapo kujihusisha na ufugaji hivyo kupitisha mifugo yao kwenye lami.
Awali akizungumza katika kikao hicho meneja wa wakala wa barabara Tanzania (TANROADS) mkoa wa Simiyu mhandisi Boniphace Mkumbo ameeleza jitihada mbalimbali wanazozifanya kukarabati barabara zilizoharibika.

Kwa upande wao baadhi ya wajumbe wa kikao hicho ,Vumi Magoti,Masunga Mizingo na Vicent Anney wakaeleza changamoto za ubovu wa barabara katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Simiyu huku wakiomba zifanyiwe matengenezo ili kurahisisha usafiri hasa kwa watumiaji wa miundombinu hiyo.