Sibuka FM

DC Simalenga ahimiza wajawazito kuhudhuria kliniki

16 March 2026, 7:13 am

Pichani ni mkuu wa wilaya ya Bariadi, Simon Simalenga akiwa kwenye moja ya shughuli za kila siku za kiserikali wilayani hapo Picha kutoka maktaba ya Sibuka fm

“Twendeni kliniki mara kwa mara kwenye vituo vyetu vya afya wakinamama wajawazito ili kujuwa hali zenu za mimba na namna ya kuwasaidia wakati wa kujifungua ili kupunguza changamoto zinazoweza kutokea wakati wa kujifungua.”

Na Daniel Manyanga 

Mkuu wa Wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu, Simon Simalenga amewataka wakina mama wajawazito  kuachana na tabia za kutokwenda kliniki kupatiwa huduma mbalimbali za kiafya jambo ambalo ameleeza kuwa limekuwa likiwasababishia changamoto mbalimbali wakati wa kujifungua.

Simalenga ametoa rai hiyo wakati akizungumza na wakazi wa kata ya Kilalo wilayani Bariadi katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi katika kituo cha afya cha Kilalo ambapo ameeleza kuwa bado kuna changamoto ya wanawake wajawazito kutokwenda kliniki wilayani humo hali ambayo imetajwa kuwasababishia shida wakati wa kujifungua.

Sauti ya mkuu wa wilaya ya Bariadi Simon Simalenga

Pilila Zambi ni mganga mkuu wa halmashauri ya wilaya ya Bariadi ambaye ameelezea hali ya wanawake kwenda kliniki pindi wanapokuwa wajawazito katika halmashauri hiyo hali inayowasaidia wahudumu wa afya kungundua mapema kama kunachangamoto kwa mama Wajawazito na namna ya kumsaidia siku ya kujifungua.

Sauti ya mganga mkuu wa halmashauri ya wilaya ya Bariadi

Wakizungumza baada ya uwekaji wa jiwe la msingi ,Masabo Matogolo,Mpejiwa Shilatu na Paschal Nsanana wakazi wa Kilalo wameeleza kuwa maboresho mbalimbali yanayofanywa na serikali katika sekta ya afya yatawasaidia wanawake kubadilika na kuanza kwenda kliniki wakati wa ujauzito.

Sauti ya wakazi wa kata ya Kilalo