Sibuka FM

Wakulima wa pamba Mkoani Simiyu wahimizwa kufuata kanuni  bora za kilimo ili kuleta tija

24 February 2026, 8:52 am

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu akipata maelezo kutoka wa viongozi wa ushirika wakati wa Mkutano mkuu wa chama kikuu cha Ushirika Mkoa wa Simiyu – SIMCU

Mimi nataka kuwa mkweli kama mpango wako wa kulima pamba ili upate kilo mia tatu (300) kwenye hekari moja afadhali nenda ukafanye kazi nyingine maana utakuwa unajitafutia umasikini ” RC Simiyu Anamringi Macha”

Na Nicholaus Machunda

Wakulima  wa zao la pamba Mkoani Simiyu wameshauliwa kufuata kanuni  bora za kilimo cha zao hilo ili kuleta tija  na kujikwamua kiuchumi  kwa kuzalisha pamba  nyingi.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe Anamringi  Macha kwenye mkutano Mkuu wa nane(8) wa Chama kikuu cha ushirika SIMCU 2018 LTD Uliofanyika wilayani Maswa

sauti ya mkuu wa mkoa wa Simiyu Mhe Anamringi Macha akizungumzia Kilimo cha Pamba

Aidha Mkuu huyo wa Mkoa,amewasisitiza wakulima kulima kilimo cha kisasa cha kufuata kanuni za kilimo na ushauri wa   watalaamu  badala ya kulima kilimo cha mazoea kinachowaletea  umasikini na kusababisha  hasara

sauti ya RC Simiyu Anamringi Macha akizungumzia kulima pamba kwa tija

Kwa upande wake, Bi, Consolata Kiluma ambaye ni naibu mrajisi wa vyama vya ushirika nchini amewaeleza wajumbe wa bodi  ya vyama vya ushirika kuwa waadilifu katika kutekeleza majukumu yao ili kuleta  ufanisi katika  Ushirika

Bi, Consolata Kiluma -Naibu Mrajisi wa vyama vya Ushirika nchini akizungumza kwenye Mkutano mkuu

Naye  Mrajisi  Msaidizi Mkoa wa Simiyu, Ndugu  Godfrey Mpepo amesema  kuwa  ushirika uko vizuri tangu kilipoanzishwa chama kikuu cha ushirika Mkoa wa Simiyu SIMCU Ltd

Ndugu Godfrey Mpepo -mrajisi msaidizi Mkoa wa Simiyu akizungumza kwenye Mkutano mkuu