Sibuka FM

Watatu wanusurika kufa moto kufuatia nyumba kuungua Bariadi

18 February 2026, 10:41 am

Pichani ni kaimu kamanda wa jeshi la zimamoto na uokoaji mkoa wa Simiyu, ASF Faustin Mtitu akizungumza na waandishi wa habari hawapo kwenye picha Picha kutoka maktaba ya Sibuka fm

Kuna majanga ambayo hanaweza kuzuilika kama tu tukiwa na utamaduni wa kuangalia mara kwa mara mfumo wa umeme wa majumbani ili kutatua changamoto za kuunguliwa kwa nyumba.”

Na,Daniel Manyanga 

Watu watatu wa mtaa wa Kidinda wilayani Bariadi mkoani Simiyu wamenusurika kifo kufuatia nyumba yao ya makazi  kuwaka moto ambapo chanzo chake kimetajwa kusababishwa na hitilafu ya umeme huku nyumba yenye vyumba vitano  kati ya vyumba hivyo  viwili  ndio vimeteketea kwa moto.

Wakizungumza na Sibuka Fm manusura hao,Joyce Komba Mama mwenye nyumba iliyoungua na Elizabeth Daniel wamesema mbali na  vyumba hivyo kuungua pia moto umeteketeza vitu vilivyokuwa ndani ya vyumba  yakiwemo magodoro, vitanda na thamani  zote huku wao wakibahatika kutoka nje mapema baada ya kuona moshi umetanda kwenye baadhi ya vyumba.

Sauti ya manusura wa tukio la kuunguliwa kwa nyumba katika mtaa wa Kidinda

Kija Bulenya na Rahel Godwin ni baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo wanasema waliona moshi ukiwa umetanda juu ya madirisha na kabla hawajafika eneo la tukio wakawasikia sauti za kuomba msaada  wa kusaidia kuzima moto huo ambao tayari ulikuwa umetanda kwenye baadhi ya vyumba.

Sauti ya mashuhuda wa tukio la moto

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kaimu kamanda wa jeshi la zimamoto na uokoaji  mkoa wa Simiyu mrakibu msaidizi wa jeshi la zimamoto na uokoaji, Faustin Mtitu amesema kuwa moto huo umeanzia kwenye vyumba vya wanapolala watoto huku akiwaomba wananchi kuwa na utaratibu wa kukagua miundombinu ya umeme kila baada ya miaka mitano ili kuweza kujuwa changamoto katika mfumo wa umeme majumbani.

Sauti ya kaimu kamanda wa jeshi la zimamoto na uokoaji mkoa wa Simiyu, ASF Faustin Mtitu