Sibuka FM

Baraza la madiwani Maswa lapitisha bil. 51 mwaka 2026/27

17 February 2026, 3:45 pm

Kwenye picha upande wa kulia ni mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Maswa, Miza Jishuli mwenye kipaza sauti akiteta jambo na mkurugenzi wa hamlashauri ya wilaya ya Maswa, Maisha Mtipa wakati wa baraza la madiwani Picha na Samwel Mwanga

Tunahitaji kuona miradi inayotekelezwa iwaguse moja kwa moja wananchi katika kuleta maendeleo kwenye maeneo yao ili kuongeza kipato cha mtu mmoja mmoja kutokana na shughuli anayoifanya”.

Na,Daniel Manyanga 

Baraza la madiwani la halmashauri ya wilaya ya Maswa mkoa wa Simiyu limepitisha rasimu ya mpango wa bajeti ya bilion 51 katika mwaka wa fedha 2026/2027 huku wakiahidi kusimamia kikamilifu ukusanyaji wa mapato pamoja na kubuni vyanzo vipya ya mapato ya ndani ili kuweza kutekeleza kikamilifu miradi ya maendeleo kwa manufaa ya wananchi.

Pichani ni mkurugenzi wa hamlashauri ya wilaya ya Maswa, Maisha Mtipa akizungumza jambo na waheshimiwa madiwani hawapo pichani wakati wa kikao hicho Picha na Samwel Mwanga

Akizungumza katika baraza hilo la bajeti lililoketi tarehe.16.02.2026 mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo,Maisha Mtipa amesema vipaumbele vya bajeti hiyo ni elimu,afya,kilimo na viwanda huku mwenyekiti wa halmashauri hiyo ambaye pia ni diwani wa kata ya Isanga,Miza Jishuli akiahidi kuzishughulikia changamoto mbalimbali zilizotajwa na mkuu wa wilaya ili kuleta maendeleo kwa wananchi.

Sauti ya mkurugenzi wa hamlashauri ya wilaya ya Maswa na mwenyekiti wa halmashauri hiyo

Julius Ikongora ni afisa mipango wa halmashauri hiyo ametaja mkakati wa ukusanyaji wa mapato ya ndani kwa ajili ya  utekelezaji wa mpango wa bajeti hiyo ni kuundwa kwa kikosi kazi kwa ajili ya ukusanyaji wa mapato katika maeneo ya minada,magulio na vituo vya kuuzia mazao na kusimamia utaratibu wa stakabadhi ghalani kuhamamisha kilimo cha mazao ya kimkakati ya biashara ya pamba,choroko,alizeti na mpunga na kuendelea na ujenzi wa vibanda 12 vya biashara katika eneo la stendi ya zamamni kwa lengo la kuongeza mapato ya ndani.

Sauti ya afisa mipango halmashauri ya wilaya ya Maswa akielezea mchanganuo wa bajeti hiyo
Picha ya pamoja ikiwaonesha madiwani wakifuatilia kwa umakini mkubwa mjadala wa bajeti katika mwaka wa fedha 2026/27 kikao kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri hiyo Picha na Samwel Mwanga

Kwa upande wao, baadhi ya madiwani walichangia mjadala huo wakitaka kuwepo kwa usimamizi madhubuti wa miradi ili kuondoa malalamiko ya ucheleweshaji na ubadhilifu wa fedha za umma ili kuharakisha kukamilika kwa miradi hiyo kwa manufaa ya wananchi ambao wanaimani kubwa na serikali yao.

Sauti ya madiwani wakichangia hoja wakati wa baraza la madiwani la kujadili na kupitisha bajeti