Sibuka FM

Maji ya kemikali ya kiwandani yaleta taaruki kwa wakazi wa Isanga

16 February 2026, 1:14 pm

Kwani sheria zetu zipo kwa ajili ya kumuhukumu nani kama kuna watu hadi leo wanatumia vibaya mamlaka na utajiri wao kuwaumiza wananchi wengine ambao hata hawana wanalolijuwa juu ya utajiri wako .”

Na,Daniel Manyanga 

Hali ya wasiwasi na hofu kubwa imetanda kwa wakazi wa kata ya Isanga wilayani Bariadi mkoani Simiyu kufuatia kiwanda cha kuchakata pamba na alizeti kutiririsha maji machafu yanayodaiwa kuwa na kemikali hivyo wameiomba serikali kuingilia kati na kuchukua hatua za haraka ili kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza.

Wakizungumza na Sibuka Fm baadhi ya wakazi hao, Mawazo Lyangala, Sitta Sayi, Paulo Lucas na Singu Ngimba wameeleza athari walizozipata hadi sasa kutokana na maji hayo ya kiwandani kutiririshwa kwenye maeneo yao.

Sauti ya wananchi wakielezea namna ambavyo walivyoathirika toka kuanza kutiririshwa kwa maji machafu hayo ya kiwandani

Sitta Masunga ni Mwenyekiti wa mtaa wa Katenga na Nashoni Ngusa ambaye ni diwani wa kata Isanga wameleeza kuwa maji hayo hadi sasa yameathiri mifugo, maeneo pamoja na mazao mbalimbali yaliyopo shambani.

Sauti ya mwenyekiti wa mtaa na diwani wa kata wakaelezea ukubwa wa changamoto

Kwa upande wake Monica Deusdedith ambaye ni afisa mazingira wa halmashauri ya mji wa Bariadi na Nkenyenge Charles Nkenyenge ambaye ni mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Bariadi wanaeleza hatua walizozichukua dhidi ya uongozi wa kiwanda hicho hadi sasa ili kukomesha tatizo hilo.

Sauti ya afisa mazingira na mwenyekiti wa halmashauri wakizungumzia hatua walichukuwa mpaka sasa