Sibuka FM
Sibuka FM
13 February 2026, 3:21 pm

“Tunamatumaini makubwa kutoka kwenu ya kuleta chachu ya mabadiliko ya tabianchi jamii ifahamu madhara yake na namna ya kukabiliana na mabadiliko hayo”.
Na,Anita Balingilaki
Mabadiliko ya tabianchi ambayo yamekuwa chanzo kikubwa cha kusababisha mafuriko na ukame kwenye maeneo mbalimbali yanatajwa kulipotezea bara la Afrika fedha nyingi ambazo zinazotumika kukabiliana na kupambana na athari za mabadiliko hayo ambayo kwa kiasi kikubwa zinagusa moja kwa moja mazingira na viumbe hai.
Wakiwa kwenye mafunzo yaliyotolewa na Media for Environment,Science,Health and Agriculture (MESHA) kwa njia ya mtandao yakizihusisha nchi sita za Afrika wataalam wamevihimiza vyombo vya habari kuwa sehemu ya kuhakikisha vinatoa mchango mkubwa wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Mafunzo hayo yametolewa na wataalam mbalimbali ambao ni Imali Ngusale ambaye ni kiongozi wa mkakati na masuala ya kiufundi African Centre for Health Climate and Gender Justice Alliance,Teresa Anderson kiongozi wa kimataifa wa haki za tabianchi kutoka ActionAid International London pamoja na Audrey Masitsa meneja mawasiliano Mission Inclusion.
Kupitia mafunzo hayo wataalam wamesema mabadiliko ya tabianchi ni suala linalolenga viumbe hai vyote na mazingira yanayovizunguka hivyo vyombo vya habari vina nafasi na mchango mkubwa katika kuongeza uelewa kwa wananchi,vinawajibu wa kufatilia ahadi zilizotolewa na serikali,utekelezaji wa ahadi hizo ikiwa ni sambamba na kuangazia vipaumbele vya sera huku wakisisitiza kuwa waandishi wa habari si watazamaji bali ni sehemu ya kukabiiliana na mabadiliko hayo kupitia taaluma yao.
Mbali na mabadiliko ya tabianchi kugusa viumbe hai vyote na mazingira ila athari kubwa zinayakumba makundi ya wanawake na watoto hususan wa kike na mabadiliko hayo hayaathiri watu wote kwa kiwango sawa na changaomoto kubwa inatokana na mifumo ikiwemo ya kijamii na kiuchumi na makundi haya (wanawake na watoto wa kike) ukumbana na majukumu mengi ikiwemo utafutaji wa maji, kuni za kupikia sambamaba na malisho kwa baadhi ya tamaduni
Yapo baadhi ya maeneo ndani ya mkoa wa Simiyu mikakati inaendelea ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kwa kupanda miti kwenye maeneo ya taasisi, pembezoni mwa mwa barabara na kwenye makazi ya wananchi lengo likiwa kurejesha uoto wa asili ambapo wananchi wanaomba zoezi hilo liwe endelevu huku viongozi wa serikali wakiitaka jamii kuwa sehemu ya zoezi la kuhifadhi mazingira.

