Sibuka FM

34% ya vifo nchini ni magonjwa yasiyoambukiza

20 January 2026, 12:26 pm

Pichani ni naibu waziri wa afya ,Dkt.Florence Samizi akizungumza jambo Picha kutoka maktaba ya Sibuka FM

Tuweni na tabia ya kupima afya zetu mara kwa mara ili kuweza kujuwa hali zetu katika kukabiliana na changamoto zozote za kiafya hali hii itasaidia sana kupunguza magonjwa yasiyo ya kuambukiza kama kisukari,presha na mengine”.

Na,Daniel Manyanga 

Asilimia 34 ya vifo nchini inachangiwa na magonjwa yasiyokuwa ya kuambukiza hali ambayo imeilazu serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania kuja na mpango wa kuboresha kitengo cha kutoa elimu ya afya kwa umma ili waweze kujikinga na magonjwa hayo ambayo ni mzigo mkubwa kwa serikali.

Hayo yamesemwa na naibu waziri wa afya,Dkt.Florence Samizi wakati akizungumza na wakazi wa wilaya ya Maswa katika hafla ya maadhimisho ya miaka 10 ya kituo cha afya cha Barikiwa  kinachomilikiwa na mzawa wa maeneo hayo na kueleza kuwa magonjwa hayo yamekuwa yakichangia vifo vya watanzania kwa asilimia 34. 

Sauti ya naibu waziri wa afya Dkt.Florence Samizi akielezea namna ambavyo serikali inatumia bajeti kubwa

Akizungumza katika maadhimisho hayo kaimu mganga mkuu wa mkoa wa Simiyu,Dr.Khamis Kulemba amesema kuwa hali ya upatikanaji wa dawa mkoani hapo umeongezeka hadi kufikia asilimia 92.12 ikilinganishwa na hapo nyuma.

Sauti ya kaimu mganga mkuu wa mkoa wa Simiyu Dr.Khamis Kulemba akizungumzia hali ya upatikanaji wa dawa

Kwa upande wake mkurugenzi wa kituo cha afya cha Barikiwa, Dkt.Ashrey Lucas ameiomba serikali iendelee kutoa ushirikiano kwenye sekta binafsi ili kuwawezesha wananchi kupata huduma za afya kwa urahisi huku wakazi wa Maswa wakipongeza hatua za kuwepo kwa kituo hicho cha afya katika kutoa huduma bora za afya.

Kwenye picha aliyekaa mbele ni mkurugenzi wa kituo cha afya cha Barikiwa, Dkt.Ashrey Lucas Picha kutoka maktaba ya Sibuka Fm
Sauti ya mkurugenzi wa kituo cha afya cha Barikiwa na wananchi