Sibuka FM

Wabunge Simiyu walia na ubovu wa miundombinu ya barabara

12 January 2026, 1:45 pm

Kwenye picha ni mkuu wa mkoa wa Simiyu, Anamringi Macha akitoa maagizo kwa TARURA na TANROADS mkoani hapo katika kuzifugulikia changamoto za barabara ili kuondoa kero kwa watumiaji Picha kutoka maktaba ya Sibuka Fm

Ndiyo kusema wakandarasi wanaojenga barabara za lami hawajui ni aina gani ya magari yanayotakiwa kutumia hiyo miundombinu au ndiyo kusema wanatimiza wajibu tu maana haiwezekani kila baada ya muda mchache tunaanza kuweka viraka hata barabara haijamaliza hata mwaka mmoja hapa wasimamizi wa wakandarasi kuna haja ya kuwa wakali.”

 Na,Daniel Manyanga 

Wakala wa barabara Tanzania (TANROADS) mkoa wa Simiyu wametakiwa kuzingatia vigezo vya watumiaji wa barabara wanazozitengeneza kupitia wakandarasi ili kuepuka uharibufu ambao umekuwa ukisababisha barabara hizo kulazimika kufanyiwa matengenezo ya mara kwa mara muda mfupi tu baada ya kukamilika pamoja na vyombo vya usafiri kupata shida baada ya  kuanza kutumia miundombinu hiyo.

Wakizungumza na Sibuka Fm wajumbe wa bodi ya barabara mkoani Simiyu akiwemo Mashimba Ndaki, Njalu Silanga na Mayala Lucas, katika kikao cha bodi hiyo kilichofanyika mjini Bariadi ambapo wameeleza namna ambavyo changamoto hiyo imekuwa kikwazo kwa watumiaji wa barabara mkoani Simiyu.

Sauti za wajumbe wa bodi ya barabara mkoani Simiyu wakielezea namna ambavyo barabara zimekuwa ni changamoto kubwa kwa watumiaji

Mhandisi Boniphace Mkumbo ni meneja wa TANROADS mkoa wa Simiyu amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo na kueleza mikakati waliyonayo ili kukabiliana nayo.

Sauti ya meneja TANROADS mkoa wa Simiyu, Mhandisi Boniphace Mkumbo akielezea hatua walizochukua kutokana na ubovu wa miundombinu hiyo

Akizungumza katika kikao hicho mkuu wa mkoa wa Simiyu Anamringi Macha akatoa melekezo ya serikali kwa TARURA na TANROADS ili kuhakikisha wanashughulikia changamoto zote za barabara mkoani Simiyu.

Sauti ya mkuu wa mkoa wa Simiyu, Anamringi Macha akitoa maagizo kwa TARURA na TANROADS