Sibuka FM
Sibuka FM
12 January 2026, 12:50 pm

“Kufuga mifugo siyo kufungo tunataka kuwaona wafugaji waone faida ya kuitwa mfugaji lazima sasa tutoke huko tuanze kufuga kwa tija ili waweze kuendesha maisha yao mazuri na familia zao ikiwemo elimu nzuri kwa watoto wao ,makazi mazuri .”
Na,Daniel Manyanga
Zaidi ya shilingi milioni 250 zimetengwa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa ajili ya kuanzisha mashamba darasa 300 katika halmashauri mbalimbali nchini ili kuwezesha wafugaji waweze kufuga kwa tija na waweze kuachana na ufugaji usiokuwa na faida.

Akizungumza na wafugaji mkoani Simiyu kwenye kikao kazi wakati wa ziara naibu waziri wa mifugo na uvuvi ,Ng’wasi Kamani amesema katika kuboresha na kuleta tija kwa wafugaji wizara hiyo imetenga kiasi cha milioni 253,000,000 kwa ajili ya kuanzisha mashamba darasa 300 ili wafugaji wapate elimu ya kufuga kwa tija na kupata malisho majira yote ya mwaka.
Wakizungumza kwenye kikao hicho cha naibu waziri baadhi ya wafugaji Chalya Seni, Shija Limbe na Shauri Machungwa wamesema kuwa changamoto ya malisho na maeneo madogo inawafanya kufuga kiholela lakini kama changamoto hizo zikifanyiwa kazi hakuna mfugaji atakayeweza kuuchukia ufugaji.
Anamringi Macha ni mkuu wa mkoa wa Simiyu amesema kuwa maeneo ya malisho yaliyopo hayatoshelezi ikilinganishwa na idadi ya mifugo iliyopo mkoani hapo hivyo kuna kila sababu za kufanya ili wafugaji wapate malisho ya kutosha