Sibuka FM
Sibuka FM
15 December 2025, 10:22 pm

Kwa sasa mpira ni ajira hivyo vijana mcheze kwa malengo kwa kujituma na nidhamu ili mfikie malengo yenu ya kucheza mbali zaidi, Lakini pia nikupongeze sana Mkurugenzi wa Hospitali ya Barikiwa kwa kutekeleza azma ya serikiali kuhusu Ushirikiano na sekta binafsi. ” Athuman Kalaghe -katibu tawala wilaya ya Maswa “
Kituo cha afya cha Barikiwa kilichopo wilayani Maswa Mkoani Simiyu kimekutanisha wananchi wa Wilaya hiyo kwa kuleta mchezo wa kirafiki wa Mpira wa Miguu kati ya Rhino Rangers ya Tabora na Barikiwa Maswa star ya mjini maswa mchezo uliochezwa katika uwanja wa ccm nguzo nane.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mchezo huo, katibu tawala wilaya ya Maswa ndugu Athuman Kalaghe ambae alikuwa mgeni rasmi amesema kuwa kwa sasa michezo ni ajira lakini pia inakutanisha watu mbalimbali huku akipongeza Uongozi wa Kituo cha afya Barikiwa kwa kuunga mkono azma ya Serikali ya kushirikiana na sekta binafsi ili kuleta maendeleo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kituo cha Afya Barikiwa Dr Ashley Lucas amesema kuwa lengo la mchezo huo ni kutengeneza ujirani mwema na kusongeza burudani kwa wananchi wa Maswa huku akisema michezo ni sehemu ya afya hivyo anashukuru uongozi wa timu ya Rhino rangers kwa kukubali kuja kucheza hapa maswa
Aidha Dr Ashley amesema kuwa kabla ya mchezo huo wachezaji wa timu ya Rhino rangers walipata nafasi ya utembelea kituo hicho cha Barikiwa na kujioneo huduma zinazotolewa pamoja na vifaa vya kisasa kabsa kwa ajili ya kusogeza huduma kwa wananchi huku akitaja huduma zinazopatikana hapo.

Alex Male ni kiongozi wa msafara wa timu ya Rhino rangers ameipongeza Hospitali ya Barikiwa kwa kuwaalika kuja kucheza mechi ya kirafiki na kusema timu ya barikiwa Maswa star ni nzuri inahitaji marekebisho madogo ili kufikia kiwango cha juu zaidi
Katika mchezo huo wa kirafiki ulihudhuriwa na wadau mbalimbali na wapenda michezo kutoka viunga vya mji wa maswa ambapo matokeo katika mchezo huo wageni Rhino rangers kutoka Tabora walishinda magori 2 na Vijana wa Barikiwa Maswa star wakipata gori 1

