Sibuka FM
Sibuka FM
23 October 2025, 5:10 pm

“Tunataka kuwa na wananchi wenye uchumi himilivu katika taifa hili ili kusaidia kupunguza umasikini uliokithili,kupunguza vifo vitokanavyo na watu kukosa pesa ya kujikimu kimatibabu ikuwa pamoja na kuondoa changamoto ya wimbi la watoto mitaani”.
Na,Daniel Manyanga
Zaidi ya milioni 156 zitokanazo na mapato ya ndani ya halmashauri katika wilaya ya Itilima mkoani Simiyu zimetolewa kama mkopo wa asilimia 10% kwa wanufaikaji 125 kwenye vikundi vya Wanawake,Vijana na Watu wenye ulemavu ili kuwainua kiuchumi katika shughuli wanazofanya.
Wakizungumza na Sibuka Fm baadhi ya wanufaikaji wa mikopo hiyo katika kundi la Vijana ,Wanawake na watu wenye ulemavu wanasema kipindi cha nyuma ambapo mikopo hiyo ilisitishwa walipata changamoto ya kupata mitaji ya kuendesha shughuli zao za ujasiliamali.
Jonathan Buluba ni kaimu afisa maendeleo ya jamii wilaya ya Itima amesema vikundi vilivyopewa mikopo ni vile vilivyokidhi vigezo huku Irene Masaki meneja mahusiano mwandamizi biashara za serikali kutoka benki ya NMB akiwaomba wale wote waliopata mikopo kuitumia kwa nidhamu na malengo yaliyokusudiwa.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Itilima, Anna Gidarya amewataka wanufaikaji wa mikopo hiyo ya asilimia kumi ya mapato ya ndani ya halmashauri kurejesha kwa wakati ili kukidhi vigezo vya kukopesheka kwa mara nyingine ikiwa ni sambamba na kuongeza wigo wa makundi mengine kukopesheka.