Sibuka FM
Sibuka FM
20 October 2025, 9:02 pm

“Kuna misemo huko mtaani kuwa mali ya serikali haina mwenyewe nataka kuwaambia kuwa haya matrekta mwenyewe yupo ukifanya unavyojuwa wewe tutakuchukulia hatua kali za kisheria”.
Na,Daniel Manyanga
Mkuu wa wilaya ya Maswa, mkoani Simiyu, Dkt.Vicent Naano Anney ameitaka bodi Pamba nchini wilayani hapo kutowapa matrekta wale wote walioharibu na kuchelewa kuwalimia wakulima wa zao pamba katika msimu wa mwaka jana wa kilimo tunapoenda kuanza msimu mpya wa mwaka 2025/2026.
Dkt.Anney ametoa maagizo hayo kwa bodi ya Pamba wakati akikabidhi trekta 50 zilizotolewa na serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania katika kukuza sekta ya kilimo ili kuongeza uzalishaji wa pamba pamoja na kupata tija kwa wakulima hao.

Dkt.Anney ameitaka bodi hiyo kuwachukulia hatua kali za kisheria wale wote watakaobainika kuiba vifaa (Spea) za trekta kutokana matukio ya mwaka jana watu kuiba spea hizo na kuuza kwingine.
Kwa upande wake mwakilishi wa bodi ya pamba wilaya ya Maswa,Ally Mabrouk amesema msimu wa kilimo cha zao la pamba 2025/2026 umeanza na wametekeleza jukumu la kuwahudumia wakulima katika ulimaji na matrekta hayo yaingie mashambani.
Nao baadhi ya madereva wa matrekta hayo wakawa na haya ya kusema.
