Sibuka FM
Sibuka FM
31 August 2025, 10:39 am

“Zoezi la chanjo ya mifugo siyo la hiari bali la lazima maana lipo kisheria na linasaidia kupunguza magonjwa ya mlipo kwa mifugo hivyo wafugaji wote muone umuhimu wa zoezi hili kwa kuipeleka mifugo yenu ikapate chanjo” DC Maswa Dkt. Vicent Anney “
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa Mkoa wa Simiyu imezindua chanjo ya mifugo kwa ajili ya kukinga mifugo dhidi ya magonjwa mbalimbali ikiwemo homa ya mapafu kwa ng’ombe
Akizindua zoezi la chanjo hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Maswa Mhe Dkt Vicent Naano Anney amesema lazima zoezi hili lisimamiwe vema ili mifugo yote ichanjwe kwani ni lazima wala siyo hiari
Mhe Anney amewashauri wafugaji kutafuta mbegu bora za mifugo ili kuleta ushindani katika soko la nyama nje ya nchi na kuongeza uchumi na tija kwa wafugaji huku akiagiza wataokaidi kuchanja mifugo yao wapelekwe Mahakamani kwa hatua za kisheria
Charles Msira ni Daktari wa Mifugo katika Halmashauri ya Wilaya ya Maswa amesema ametaja idadi ya mifugo na malengo waliyojiwekea katika kufanikisha zoezi hilo la uchanjaji wa mifugo
Msira amesema kuwa chanjo hii ni muhimu kwa mifugo kwani itaenda kudhibiti milipuko ya magonjwa ya mifugo, kuongeza uzalishaji wa mazao ya mifugo yenye ubora na salama kwa watumiaji huku akitaja hasara za kutochanja mifugo.
Nao baadhi ya wafugaji wa kata ya Nyabubinza wakaelezea furaha yao baada ya kuletewa huduma ya chanjo kwa hapo awali walikuwa wanapoteza mifugo kutokana na magonjwa mbalimbali na kutumia fedha nyingi kutibu mifugo yao

