Sibuka FM
Sibuka FM
26 August 2025, 12:06 pm

Uraghbishi siyo mradi, Uraghbishi ni Maisha ya kila siku yakubadilisha fikira na mitazamo ya Jamii katika ushiriki na utatuzi wa changamoto zinazowakabili katika Jamii maana hamna siku changamoto zitaisha katika hivyo wananchi wawe na uwezo wa kuzitatua wao wenyewe, lengo ni kupunguza utegemezi wa wananchi kwa Serikali na kuongeza ushiriki wa shughuli za maendeleo-” Marius Isavika -Kasodefo
Zaidi ya Waraghbishi 40 Wilayani Maswa Mkoani Simiyu wamepewa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kushiriki katika miradi mbalimbali ya maendeleo katika Jamii zao
Mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Shirika la Kawiye Social Development Foundation (Kasodefo) kwa kushirikiana na Shirika la Twaweza yakiwa na lengo kuamsha ari ya jamii katika kupanga , kuibua na kushiriki utekelezaji wa vipaombele vya maendeleo katika Jamii zao.
Marius Isavika ni Mratibu kutoka Shirika la Kasodefo amesema kuwa mafunzo hayo yataenda kuondoa utegemezi wa wananchi kwa Serikali, kuongeza ushiriki katika masula ya maendeleo pamoja na kuongeza uwajibikaji
Aidha Isavika ameongeza kuwa wamewajengea uwezo wa kutumia vyombo vya habari na Teknolojia ya habari katika kutangaza kazi za Uraghbishi ili kufikia watu wengine zaidi

Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wameeleza namna wanavyoshirikiana na viongozi wa Serikali ya Kijiji na Wananchi katika Kuibua, Kupanga na kushiriki namna ya kutatua changamoto zinazowakabili katika maeneo yao

