Sibuka FM
Sibuka FM
14 August 2025, 5:26 pm

Chama cha Ukombozi wa Umma siyo chama kigeni, ni chama kikongwe ila kilikuwa kinatambulika zaidi ngazi za Juu lakini kwa sasa tumeamua kukishusha ngazi za chini kabisa kwa wananchi wakitambue na kukipa ridhaa “Gimbi Masaba -Mratibu wa Uchaguzi Chaumma kanda ya Serengeti “
Chama cha ukombozi wa Umma (chaumma ) kimesema kuwa imejipanga kikamilifu kushiriki Uchaguzi mkuu wa Rais , Wabunge na Madiwani utaofanyika mwishoni mwa mwezi Oktoba mwaka 2025 huku sera yake ikiwa ni kuimarisha Afya na Lishe kwa Watanzania
Hayo yamesemwa na mratibu wa uchaguzi chaumma kanda ya Serengeti Bi Gimbi Dotto Masaba wakati wa Ziara ya kutambulisha chama hicho kwa wananchi wa Maswa Mkoani Simiyu huku akiomba watanzania na wana Maswa kukiunga mkono ili kiweze kuleta Ukombozi kwa wananchi
Masaba amesema kuwa wameamua kutoka chadema na kujiunga na chaumma ili washiriki uchaguzi mkuuu na kudai mabadiliko wakiwa na wawakilishi katika ngazi za maamuzi ikiwemo Bungeni huku akisema Vijana wengi wamejitokeza kuchukua fomu ili waweze kuleta mabadiliko

Kwa upande wake mratibu wa uchaguzi Mkoa wa Simiyu Bi Kwandu Mpanduzi amesema kuwa chaumma kimedhamilia kwenda kutetea wakulima hasa wa zao la pamba ambalo limekuwa na kizungumkuti na manyanyaso kwa wakulima kutokana na zao hilo kufanywa na Wabunge ambao ndio watunga sera
Flora Masuke na James Mahangi ni watia nia wa Ubunge jimbo la Maswa mashariki kupitia chama cha Chaumma wameahidi kuleta Mabadiliko kwa Maswa endapo wananchi wataunga mkono na kuwachagua



