Sibuka FM

Vigogo wa migodi waenguliwa kwenye nafasi zao Simiyu

3 July 2025, 8:25 pm

Kwenye picha ni mkaguzi mkuu wa migodi nchini mhandisi Hamis Kamando akizungumza jambo na wachimbaji wadogo wa madini na wadau wa sekta hiyo katika mafunzo ya usalama kwa wachimbaji wadogo wakiwa wanatekeleza majukumu yao Picha kutoka maktaba ya Sibuka Fm

Hatuwezi kufikia malengo kwa sitaili hii lazima tuheshimiane kwa kuzingatia sheria,miongozo na miiko ya kazi hivyo lazima katika safari ya mafanikio kuna watu tunapaswa tuachane nao kabisa ili safari hii iweze kwenda mbele kwa kasi tunayotakiwa ili kufikia malengo ya nchi”.

 Na, Daniel Manyanga 

Mkaguzi mkuu wa migodi nchini Mhandisi,Hamis Kamando ametengua uteuzi wa mameneja wote wa migodi midogo waliopo katika mkoa Simiyu kutokana na kuonesha utovu wa nidhamu katika kutekeleza majukumu yao ya kazi walizopangiwa.

Mhandisi Hamis Kamando amechukua uamuzi huo wakati akizungumza na wachimbaji wadogo wa madini na wadau wa sekta hiyo kutoka mikoa ya Simiyu na Mara kwenye mafunzo ya usalama kwa wachimbaji wadogo madini wakiwa wanatekeleza majukumu yao ya uchimbaji mafunzo yaliyofanyika mjini Bariadi mkoani Simiyu.

Mhandisi Kamando amesema kuwa haiwezekani serikali inatumia gharama kubwa katika kuandaa mafunzo haya halafu kuna watu wanatokea wanataka kukwamisha shughuli kwa kushindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo pamoja na kuonesha utovu wa nidhamu wakati wa majukumu waliyopangiwa kufanya.

Sauti ya mkaguzi mkuu wa migodi nchini, mhandisi Hamis Kamando akizungumzia chanzo cha kuwapiga chini viongozi wa migodi ya madini
Picha ya pamoja ikiwaonesha wachimbaji wadogo wa madini na wadau wa sekta hiyo wakiwa wanafuatilia jambo wakati wa mafunzo ya usalama migodini Picha kutoka maktaba ya Sibuka Fm