Sibuka FM
Sibuka FM
1 July 2025, 5:12 pm

“Bado tunasafari kubwa sana katika kuelimisha jamii ya watoa huduma wa dawa muhimu za binadamu maana wengi wao wanakiuka mashariti ya leseni zao bahati mbaya sana hata wanaohudumiwa nao wanaingia kwenye makosa yale yale”.
Na, Daniel Manyanga
Mamlaka ya dawa na vifaa tiba TMDA kanda ya ziwa mashariki amewataka wamiliki na wauzaji wa maduka ya dawa muhimu za binadamu kufuata sheria, kanuni , taratibu na miongozo ya uendeshaji wa maduka hayo Ili kujiepusha na mkono wa sheria kutokana na makosa ya ukiukwaji wa leseni zao walizopewa na mamlaka husika.

Hayo yamesemwa na kaimu meneja wa mamlaka ya dawa na vifaa tiba TMDA kanda ya ziwa mashariki ,Aggrey Muhabuki wakati akizungumza na wauzaji pamoja na wamiliki wa maduka katika halmashauri ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu na kueleza kuwa maduka ya dawa muhimu yamekuwa yakitumika kinyume na mashariti ya leseni.
Muhabuki ameongeza kuwa Kuna maduka mengine wanalaza wagonjwa ambapo ni kinyume cha sheria kulingana na leseni walizopewa na mamlaka husika hivyo amewataka wamiliki wa maduka hayo kufuata miongozo wanayopewa.
Aziza Hamis ni katibu wa afya wa mkoa wa Simiyu ambaye amevitaja vitendo vya ukiukwaji wa sheria vinavyofanywa katika maduka ya dawa muhimu mkoani Simiyu huku kaimu mfamasia wa mkoa wa Simiyu ,Philemon Mtinda akieleza kuwa hatua zinazochukuliwa kwa wauzaji wanaokiuka sheria zimesaidia kurekebisha mienendo yao.
Baadhi ya wamiliki wa maduka ya dawa muhimu mkoani Simiyu wameshaurielimu itolewe zaidi hususan maeneo ya vijijini ili kuwasaidia wananchi kuwa na uelewa juu ya huduma sahihi wanazopaswa kuzipata katika maduka ya dawa muhimu.