Sibuka FM
Sibuka FM
30 June 2025, 6:52 pm

“Twendeni tukatende haki kwa kuzingatia miiko ya taaluma zetu pale ambapo tunatekeleza majukumu ya ubora wa bidhaa ambazo zipo sokoni bila kukandamiza wafanyabiashara wanaolalamikia utendaji kazi wakati wa ukaguzi”.
Na, Daniel Manyanga
Wafamasia, wataalam wa maabara na maafisa mifugo katika halmashauri za mkoa wa Simiyu wametakiwa kuzingatia maadili ya kaguzi mbalimbali ambazo wanazozifanya kwa wauzaji wa maduka ya dawa muhimu ya yale ya pembejeo za kilimo na mifugo ili kuhakikisha wanafanya kazi yao kwa ufanisi na kuisaidia jamii kupata huduma bora na stahiki kutoka katika maduka hayo ili kuondoa minong’ono ya wafanyabiashara wanaowalaumu.

Akizungumza na wakaguzi hao wakati wa semina elekezi ya siku moja mjini Bariadi katibu wa afya wa mkoa wa Simiyu,Aziza Hamis ambapo amewataka kuzingatia weledi wa taaluma yao na miiko ya kazi katika kaguzi wanazozifanya.
Venance Bulushi ni mkaguzi mwandamizi wa dawa na vifaa tiba kutoka mamlaka ya dawa na vifaa tiba TMDA kanda ya ziwa mashariki, amewataka wakaguzi hao kuzingatia sheria katika ukaguzi wao, ili kudhibiti ubora wa bidhaa za dawa na vifaa tiba zilizopo sokoni.
Victor Chengula ambaye ni mfamasia wa wilaya ya Maswa na Colnel Masinde ambaye ni daktari wa mifugo kutoka wilaya ya Itilima ni baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo,wameeleza yatakavyowasaidia kuboresha utendaji wao wa kazi na kuongeza ufanisi zaidi.