Sibuka FM
Sibuka FM
28 May 2025, 7:51 pm

“Kumaliza rushwa hapa nchini ni changamoto kubwa sana maana hata watumishi umma waliokula kiapo cha uaminifu ndiyo wanakuwa watu na viongozi wa kwanza katika kutekeleza ubadhilifu wa mali za umma halafu hao hao ndiyo wanahimiza uzalendo haya ni maajabu kweli”.
Na, Daniel Manyanga
Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini (TAKUKURU) mkoa wa Simiyu imeokoa zaidi ya bilioni sita za miradi ya sekta ya elimu iliyojengwa chini ya kiwango katika miradi inayotekelezwa mkoani hapo kutokana na fedha zilizoletwa na serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania katika kuboresha miundombinu ya elimu.

Hayo yamesemwa na mkuu wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini (TAKUKURU) mkoa wa Simiyu ,Manyama Tungaraza wakati akitoa taarifa ya kipindi cha robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2024/25 ofisini kwake mbele ya waandishi wa habari.
Manyama amesema kuwa mradi wa shule ya sekondari ya wavulana Simiyu ambapo baadhi ya miundombinu ya mradi kujengwa juu ya bomba la maji safi hatua iliyopelekea mradi huo kuchelewa kwa takribani siku 119.