Sibuka FM
Sibuka FM
27 May 2025, 11:19 am

“Uchumi wetu unajengwa na wajasiliamali wadogo wadogo hivyo tuna kila sababu kwa mamlaka husika kuwatengenezea mazingira mazuri ya wao kufanya biashara ikiwemo miundombinu ya masoko pamoja na kuangalia tozo ambazo hazina afya kwa wafanyabiashara”.
Na, Daniel Manyanga
Kukosekana kwa soko la uhakika la kufanyia biashara kwa wakazi wa mji mdogo wa Sangamwalugesha uliopo kata ya Sangamwalugesha wilayani Maswa mkoani Simiyu kumetajwa kuchangia kudorora kwa biashara maeneo hivyo wameomba kujengewa soko ili waweze kuuza, kununua bidhaa mbalimbali hali ambayo itakuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na jamii nzima ya maeneo jirani.
Doto Salum ni mkazi wa kijiji hicho amewasilisha hoja hiyo mbele ya mkuu wa wilaya ya Maswa wakati wa mkutano wa hadhara na wananchi ambapo ameuliza swali kwa nini mji huo mdogo hauna soko la uhakika licha ya kwamba eneo lipo la kujengewa miundombinu hiyo ili iwe rahisi kwa wafanyabiashara kufanya biashara zako kwa uhakika tofauti na hivi sasa wanauzia majumbani kwao.
Doto Salum na Dadas Maulid wamesema kuwa uwepo wa soko hilo kuwasaidia kununua ,kuuza na kufanyabiashara hali itakayoondoa wafanyabiashara makanjanja wenye kuwaibia wakulima na wauzaji pamoja kuongeza kipato cha mtu mmoja mmoja na jamii nzima ya maeneo jirani.
Akijibu changamoto hiyo mkurugenzi mtendaji wa halmshauri hiyo, Maisha Mtipa akaahidi kulifanyia kazi swala hilo hivyo wananchi wawe na uvumilivu wakati serikali inatafuta namna bora ya kuwa soko maeneo hayo.