Sibuka FM

Katakata ya umeme Simiyu yawaibua wananchi

21 May 2025, 4:02 pm

Kwenye picha ni muonekano wa bwawa la Mwalimu Nyerere moja wapo wa mradi mkubwa wa umeme ambao utaondoa kabisa hiyo adha ya kukatika kwa umeme mara kwa mara mradi unaotekelezwa na serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania Picha kutoka maktaba ya Sibuka Fm

‘‘Tunahitaji nishati ya umeme ya kutosha mahitaji yetu ni kweli juhudi ni kubwa sana zinazofanywa na kiongozi wetu mkuu wa nchi hii Rais ,Mhe,Dkt.Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha wananchi wanapata umeme wa kutosha ili waweze kuongeza uzalishaji mali na kujiongezea kipata kwa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla wake’’.

Na,Daniel Manyanga

Wananchi  mkoani Simiyu wameonyesha kukerwa na kukatika kwa huduma za umeme mara kwa mara kwenye maeneo ya makazi na biashara hali ambayo wametaja kukwamisha shughuli mbalimbali za uzalishaji mali zinazotegemea umeme hivyo kuigia hasara kwa kuamua kutumia nishati mbadala ili shughuli zisisimame.

Wakizungumza na Sibuka Fm kwa nyakati tofauti Zebedayo Kingi na Kasili Kitebo ambao ni wakazi wa mkoa wa Simiyu wameeleza namna ambavyo changamoto hiyo inakwamisha shughuli mbalimbali za kiuchumi wanazozifanya za kujiongezea kipato ili kiweze kuwasaidia kuendesha maisha yao hivyo kulazimika kutumia njia nyingine katika kuendesha shughuli zinazotumia umeme.

Sauti ya wananchi wakizungumza namna ambayo katakata ya umeme inavyokwamisha shughuli za uzalishaji zinazotumia umeme
Kwenye picha ni muonekano wa mradi wa kupoza umeme inayotekelezwa na serikali ili kuwa na nishati ya uhakika kwa wananchi wake Picha kutoka maktaba ya Sibuka Fm

Akijibia changamoto hiyo ya kukatika kwa umeme mara kwa mara mkuu wa mkoa wa Simiyu, Kenani Kihongosi ameeleza jitihada zinazofanywa na serikali kwa ajili ya kuhakikisha changamoto hiyo inaondolewa mkoani Simiyu hali ambayo itaondoa kero kwa wananchi ambao ni wahanga wakubwa katika hili.

Sauti ya mkuu wa mkoa wa Simiyu, Kenani Kihongosi akielezea jitihada zinazofanywa na serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania katika kumaliza hiyo shida ili wananchi waweze kujikita zaidi kwenye uzalishaji