Sibuka FM
Sibuka FM
20 May 2025, 4:27 pm

Lengo la Kongamano hili la Baraza la Amani ni kuwakutanisha Viongozi mbalimbali wa Dini na kukumbushana nafasi ya Viongozi hao katika kuleta amani hasa kuelekea uchaguzi mkuu utaofanyika mwaka huu pamoja na kuombea Rais Samia anapoongoza taifa kubwa kama Tanzania
Wajumbe wa Baraza la Amani Wilayani Maswa, mkoani Simiyu wamefanya Kongamano la kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan pamoja na Uchaguzi Mkuu utaofanyia mwezi Oktoba, 2025
Wajumbe hao kutoka Makundi mbalimbali ya Viongozi wa Dini, Wazee maarufu, Viongozi wa Kisiasa, Viongozi wa Tiba asili na Viongozi wa Serikali lengo ni kuhakikisha amani ya Nchi inadumishwa hasa kuelekea kipindi ya Uchaguzi Mkuu utakaofanyi mwishoni mwa mwaka huu 2025
Akimkaribisha mgeni rasmi katika Kongamano hilo baada ya majadiliano ya ndani, mwenyekiti wa kamati hiyo ya Amani wilayani Maswa ambaye pia ni Shekhe wa Wilaya , shekhe Issa Elias amesema kuwa yote waliyokubaliana wakayaseme kwa waumini wao huko Makanisan na Misikitini ili kila mmoja awe mlinzi wa Amani katika eneo lake.
Dkt Vicent Naano Anney ni Mkuu wa Wilaya ya Maswa amesema suala la kulinda na utunza amani ni lamuhimu sana hasa tunapoelekea kipindi cha Uchaguzi mkuu na siyo kuwa sehemu ya uvunjivu wa amani maana yapo mataifa yanatamani amani tuliyonayo sisi Watanzania

Aidha Mhe Anney amesisitiza waandishi wa habari kuwa na ueledi na Uzalendo katika kuandika habari na siyo kila wakati kuandika mabaya tu na Uchonganishi katika ya Serikali na Wananchi wake
Akitoa taarifa kwa niaba ya mwenyekiti, katibu wa Baraza la Amani na katibu wa Bakwata wilayani hapa, Maulid Amir Mlete amesema ni vizuri kutafakari kwa kina kuhusu Tunu za taifa ambazo ndio dira za nguzo na utulivu ambao ziliasisiwa na viongozi wetu wa taifa hili
Kwa upande wake mwenyekiti wa Parokia ya Nyalikungu wilayani Maswa Mwl Kilama Mwesiga amesema viongozi wa Dini wanayonafasi kubwa ya kuleta amani na utulivu kwa kuzingatia Haki na Utu wani mkiwatendea haki wananchi manung’uniko na chuki zitapungua
Onesmo Makota ni Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi (ccm) Wilayani hapa amesema tusikubali watu wachache watushawishi kuvunja amani na kutufitinisha kwani baada ya uchaguzi maisha yataendelea huku akisema ccm itakuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha amani inatawala.


