Sibuka FM
Sibuka FM
6 May 2025, 6:17 pm

‘‘Hatuwezi kuwa na taifa lenye uchumi mkubwa kama watu wake wako wanapambana na changamoto ya miundombinu ya afya lazima kwanza tujali afya za watu ambao ndiyo nguvu kazi ya kuyafikia hayo maendeleo ni kweli tumefanya mageuzi makubwa sana katika sekta ya afya sasa kilichobaki ni kuona maendeleo yanaenda kwa kasi ya 5G ili kuyafikia malengo ya viongozi wetu wa kitaifa’’.
Na,Daniel Manyanga
Wakazi wa maeneo mbalimbali mkoani Simiyu wameeleza kuwa uzalishaji wa hewa tiba (Oksijeni) katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Simiyu, umewasaidia kuondokana na adha mbalimbali walizokuwa wakizipata kipindi cha nyuma,ikiwemo gharama kubwa za matibabu pindi mgonjwa anapohitaji huduma hiyo ya matibabu ambapo iliwalazimu kufunga safari ya kwenda katika hospitali ya rufaa ya kanda ya Bugando na sehemu zingine.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti tofati na Sibuka Fm,Yohana Isamla, Sabrina Chales na Godfrey Samuel ambao ni wakazi wa mkoa wa Simiyu wameeleza changamoto walizokuwa wakizipata kabla ya hewa tiba hiyo kuanza kuzalishwa hospitalini hapo.
Dk. Juma Muna ni mratibu wa huduma za tiba katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Simiyu na hapa anaeleza namna ambavyo uzalishaji huo wa hewa tiba umekuwa msaada kwa wagonjwa wanaohitaji huduma hiyo huku mhandisi wa vifaa wa hospitali hiyo, Bathromeo Kapuga akieliza hali ya uzalishaji wa hewa tiba hiyo hospitalini hapo.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Simiyu Kenani Kihongosi, ameeleza namna ambavyo serikali imefanya maboresho ya huduma za afya katika mkoa wa Simiyu katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan ambapo ameleta fedha nyingi ambazo zimefanya mageuzi makubwa kwenye sekta ya afya.