Sibuka FM
Sibuka FM
26 April 2025, 6:40 pm

Muungano ni Tunu ya Taifa hivyo hatuna budi kuulinda na kuudumisha na kuwapuuza wale wachache wanaoleta chokochoko juu ya Jamhuri ya Muungano wetu wa Tanzania ” DC Maswa Mh Dkt Vicent Naano wakati akifungua Bonanza la Maadhimisho ya sherehe za miaka 61 ya Muungano”
Na Nicholaus Machunda
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa, Mkoani Simiyu imesherekea kitofauti miaka 61 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kuunda Tanzania kwa kufanya Bonanza la Michezo mbalimbali ikiwemo Mpira wa Miguu, kuvuta kamba, Kukimbia na Magunia, Kunywa soda na Mkate Pamoja na kucheza mziki,
Akifungua bonanza hilo , Mkuu wa Wilaya ya Maswa Mhe Dkt Vicent Naano Anney amesema kuwa Muungano ni Tunu ya Taifa hivyo hatuna budi kuulinda na kuudumisha na kuwapuuza wale wachache wanaoleta chokochoko juu ya Jamhuri ya Muungano wetu wa Tanzania
Mhe Dkt Naano ameongeza kuwa ni vizuri kuwa na mwendelezo wa Bonanza kila mwisho wa Mwezi ili Mji uweze kuchangamka huku akiahidi kuanzisha Ligi yake itakayoitwa Samia Cup kwa kushirikisha makundi mbali mbali ili Mji uchangamke na watu kufanya biashara mbalimbali.

Saidi John Mshana ni Afisa Utamaduni na Michezo Halmashauri ya Wilaya ya Maswa ametaja Michezo mbalimbali iliyofanyika katika Bonanza hilo la kusherekea Miaka 61 ya Muungano wa Tanzania lililokuwa limefana kutokana na Ubunifu wa Michezo mbalimbali
Aidha Mshana amesema kuwa kutakuwa na mwendelezo wa Bonanza kila mwezi kama alivyoagiza Mkuu wa Wilaya kwa lengo la wananchi kushiriki kufanya Mazoezi ili kujiepusha ya Magonjwa yasiyo ya kuambukizwa

Baadhi ya Wananchi walioshiriki bonanza hilo Wamewashukuru Viongozi wa Wilaya kwa Kuandaa michezo hiyo kwani imewaweka karibu pamoja na ushirikiano kati ya Wanachi na Viongozi wa Serikali
Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa Ndugu Vivian Christian amewashuru Watumishi, Taasisi na Wananchi kwa kushiriki Bonanza la sherehe za Muungano huu akiwaalika kujitokeza kwa Wingi katika Sherehe za Siku ya Wafanyakazi (Mei Mosi ) ambapo kimkoa zitafanyika Wilayani Maswa

