

1 April 2025, 5:27 pm
“Maneno ya wanasiasa yenye viashiria vya uvunjifu wa amani yasipuuzwe lazima tuweze kuchukua hatua kwa hao viongozi maana amani tuliyonayo Kuna nchi zingine huko kila kukicha wanatafuta amani na hawajui lini wataipata hiyo amani fikra zangu tu ivi kwani sheria zinasemaje kwa watu wa namna hii wenye kauli chonganishi?.”
Na, Daniel Manyanga
Viongozi wa dini ya Kiislamu mkoani Simiyu wameiomba jamii wakiwemo waumini wa dini hiyo kuendelea kudumisha amani ya nchi iliyopo na wasiwe sehemu ya kusikiliza maneno ya baadhi ya wanasiasa ambayo yanaviashiria vya uvunjifu wa amani wanapokuwa kwenye majukwaa ya kisiasa.
Wito huo umetolewa na Sheikh wa mkoa wa Simiyu,Issa Kwezi wakati akizungumza na waumini wa dini hiyo mjini Bariadi.
Sheikh Kwezi amewaomba waislamu na wananchi mkoani hapo kuwa sehemu ya kusababisha watu wengine waishi kwa amani na kuendelea kujivunia tunu hiyo.
Dotto Mayombi,Rukia Juma na Hamida Shaban ni waumini wa dini hiyo wameahidi kuyaishi yale yote waliopewa na viongozi wao.