

27 March 2025, 9:28 am
Lengo la Mikopo hii ni kuwakomboa watanzania kiuchumi na hivyo muwe waaminifu katika Marejesho ya Mikopo yenu mliyopewa ili watanzania wengine waendelee kukopa na siyo kwenda kunywea Pombe na kununua Vitenge “Dc Maswa Dkt Vicent Naano “
Zaidi ya shilingi Milioni 173 zimetoewa na Halmashauri ya Wilaya ya Maswa kwa Vikundi 15 vya Uzalishaji Mali vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu kama gawio la asilimia 10 ya Mapato ya ndani ya Halmashauri.
Akizungumza na wana vikundi waliopokea Mkopo huo, Mkuu wa Wilaya ya Maswa Dkt Vicent Naano Anney amesema kuwa lengo la Mikopo hiyo ni kuwakomboa watanzania kiuchumi na kuwataka kuwa waaminifu katika Marejesho ili watanzania wengine waendelee kukopa
Aidha Dkt Vicent Naano amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri kuhakikisha wote waliokopa na wakashindwa kurejesha wasakwe na wakatwe kisha wapelekwe Mahakamani ili waweze kurejesha fedha hizo ili Vikundi vingine waendelee kukopa na kujikwamua Kiuchumi
Akitoa taarifa kwa Mgeni rasmi, Kaimu mkuu wa Divisheni ya Maendeleo ya Jamii wilayani hapa Bi Basila Bruno amesema kuwa jumla ya Vikundi 15 vya Wanawake, Vijana na watu wenye Ulemavu vyenye wananchama 105 wamepatiwa Mikopo hiyo kwa awamu ya kwanza.
Robert Urassa ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Maswa amesema kuwa hategemei kuona vikundi hivyo mwakani vinaomba mikopo tena na badala yake mitaji hiyo iwasaidie kuwainua zaidi kiuchumi na kutoa marejesho ili waendelee kutoa mikopo kwa vikundi vingine.
Akimwakilisha Mbunge wa Jimbo la Maswa Mashariki Mhe Stanstaus Nyongo, Marco Bukwimba ni katibu wa Mbuge amewataka walengwa waliopata Mikopo kwenda kutekeleza waliyoelekezwa na wataalamu ili fedha hizo ziwanufaishe na siyo kwenda kulewa Mvinyo na kununua vitenge
Katika hafla hiyo ya kukabidhi Mikopo kwa Vikundi vya Uzalishaji mali vya Wanawake, Vijana na Wenye Ulemavu imehudhuriwa na mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mhe, Paul Maige na kuwataka walengwa kwenda kusimamia malengo yao ili fedha hizo zilete matokeo tarajiwa
Baadhi ya walengwa wa Vikundi waliopata Mikopo hiyo (Elias Emmanuel na Zawadi Pima ) wameishukuru Serikali ya Mhe, Rais Dkt Samia Suluhu Hasani kwa kutoa mikopo hiyo kwani itaenda kuwainua Kiuchumi huku wakiahidi kurejesha kwa wakati ili vikundi vingine waweze kukopeshwa.