

15 February 2025, 12:40 pm
‘‘Kilimo ni moja wapo ya sekta ambayo imeajiri watu wengi sana na nimuhimu sana katika ujenzi wa taifa maana hatuwezi kuwa na uchumi imara wakati watu wake wanalia njaa hiyo siyo ajenda ya taifa lazima wakulima tuwalinde na kuwapa thamani kutokana na kazi kubwa wanayoifanya ya kuzalisha chakula’’.
Na,Daniel Manyanga
Wakulima wa zao la choroko wilayani Maswa mkoani Simiyu wameishukuru serikali mkoani humo kwa kuanzisha mfumo wa stakabadhi ghalani katika uuzaji wa zao hilo mfumo ambao wameeleza kuwa unawanufaisha kwa kiasi kikubwa ikilinganishwa na hapo awali kabla ya matumizi ya mfumo huo kuanza.
Wakizungumza Sibuka fm kwa nyakati tofauti wakulima hao wameeleza manufaa wanayoyapata kwa sasa katika uuzaji wa mazao yao kupitia stakabadhi ghalani kufuatia serikali mkoani hapo kuanza kutumia mfumo huo hali ambayo inalengo la kuwainua wakulima kutokana na kazi kubwa wanaifanya wakati wa msimu wa kilimo.
Wamesema kuwa mwanzoni mkulima alikuwa hapewi thamani kubwa kama leo hii kutokana na mfumo huo wa uuzaji wa zamani kuwaibia wakulima hali ambayo iliwafanya wengine kuangalia namna nyingine ya kuachana na kilimo lakini ujio wa stakabadhi ghalani utawafanya walime kwa tija.
Kwa upande wake ,Ntemi Mpina ambaye ni mmoja wa wafanyabiashara ya mazao mbalimbali ya nafaka wilayani Maswa ambayo kwa sasa yanauzwa kwa kutumia mfumo wa stakabadhi ghalani ameeleza faida za matumizi ya mfumo huo.